Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo,
Yohanes Nyoni alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu
ya tukio hilo ambapo alieleza kuwa lilitokea Machi 6 mwaka huu katika kata
hiyo.
Nyoni alifafanua kuwa sababu kubwa iliyosababisha mradi huo
kuharibiwa na mafuriko hayo inatokana na uchafuzi wa mazingira katika chanzo hicho
cha maji kwani baadhi ya wananchi wameweka makazi ya kudumu karibu na chanzo na
kuendesha shughuli za kilimo.
Alisema kuwa hali hiyo husababisha nyakati za masika udongo
kumomonyoka hatimaye matope hujaa kwenye chanzo na mawe makubwa yaliyobebwa na
mafuriko kuvunja miundombinu husika ya mtego wa maji kutokana na kukosekana kwa
uimara wa ardhi.
Pia alieleza kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi hao kukata
miti rafiki ya maji na ambayo pia imekuwa ikitunza ardhi inayozunguka chanzo
hicho jambo ambalo husababisha chanzo kuzolewa na wananchi kukosa maji.
Alisema kuwa timu ya wataalamu imekwenda katika eneo la tukio
na kubaini uharibifu huo ambapo wameshauri kwamba katika kuweza kuwanusuru
wananchi wa Kigonsera kukosa maji kwa muda mrefu ni vyema sasa, yakachukuliwa
maji kutoka chanzo cha Mkako na kuyagawa katika sehemu mbili ili kuweza kulisha
wananchi hao kwa muda wakati upembezi yakinifu ukiendelea kufanyika juu ya
kukarabati chanzo hicho kilichoharibiwa na mafuriko hayo.
Vilevile aliongeza kuwa tathimini iliyofanyika ili kuweza
kunusuru hali hiyo imebainika kuwa kutoka kwenye mtandao mkuu wa mradi wa maji
Mkako mpaka katika mtandao mkuu wa maji Kigonsera baada ya kufanya vipimo vya
umbali wa bomba, ujenzi wake pamoja na usimamizi jumla ya shilingi milioni
5,685,000 zinahitajika ili maji yaweze kufika kwenye matenki ya kuhifadhia maji
katika mradi wa maji Kigonsera.
Endapo zitapatikana fedha hizo na kazi hiyo kufanyika,
wananchi hao watakuwa wameondokana na tatizo la upatikanaji wa maji safi na
salama.
Kwa ujumla mradi wa maji Kigonsera ambao umeharibiwa na
mafuriko ya mvua ulianza kujengwa mwezi Agosti mwaka 2012 na kukamilika ujenzi
wake mwezi Machi 2013 chini ya Mpango wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)
ambapo uligharimu shilingi milioni 479,153,257 ikiwa ni gharama za ujenzi wa
mradi wote.
No comments:
Post a Comment