Beatrice Ndomba, akiwa bado hajapata tatizo la ulemavu wa miguu. |
Na Albano Midelo,
Songea.
HUJAFA hujaumbika, Beatrice Ndomba (24)
pichani, alizaliwa akiwa na miguu yake yote miwili hadi alipomaliza kidato cha
nne na kuanza kusoma Stashahada ya uhasibu mwaka wa kwanza mkoani Mbeya 2014.
Aidha akiwa huko ndipo alipatwa na ulemavu
wa viungo baada ya kukatwa miguu yake yote miwili.
Beatrice hivi sasa anaishi mtaa wa Ruhuwiko
kanisani, katika Manispaa ya Songea mkoa wa Ruvuma na ndoto zake za kuwa
Mhasibu zimefifia.
Mwaka jana alipata mafunzo ya ufundi kushona, kwa hiyo amejiajiri
kama fundi cherehani na kwamba hivi sasa anahitaji msaada wa miguu bandia, ili
aweze kutembea na kuendesha shughuli zake za kujitafutia ridhiki kama Watanzania
wengine.
Beatrice ni mtoto yatima, anaishi na wadogo
zake wawili, ukiguswa na tatizo hili unaombwa kumchangia kiasi chochote kile ili
aweze kununua viungo bandia vyenye ubora kwa kuwa alivyonavyo sasa vinamuumiza miguu na hawezi kutembea vizuri.
Mawasiliano yake anapatikana kwa simu namba 0766
642634 au 0673 054535.
No comments:
Post a Comment