Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
Dkt. Mahenge alionekana kuwa mkali na kusikitishwa na hali
hiyo huku akishangazwa na wakandarasi hao kulipwa fedha kwa baadhi ya kazi
walizofanya huku hatua ya utekelezaji ikiwa bado haijakamilika kwa viwango
vinavyotakiwa.
“Hivi sasa naweza nikawaweka ndani tokea barabara hii ianze
kujengwa hadi sasa haijakamilika, naagiza viongozi ngazi ya mkoa na wilaya ya
Mbinga kwa kushirikiana na Katibu tawala wa mkoa huu fanyeni uchunguzi wa kina
juu ya kazi hii ikiwemo na malipo yaliyofanyika, kwani inaonesha ni
uchakachuaji mtupu umefanyika na tukibaini haya maovu mliyoyafanya tutawaweka
ndani wote watakaokuwa wamehusika kuhujumu mradi huu na kuwafikisha kwenye
vyombo vya kisheria”, alisema Dkt. Mahenge.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka pia viongozi wa wilaya ya Mbinga
kuwa na mazoea ya kutembelea miradi ya maendeleo ya wananchi ambayo
inatekelezwa katika maeneo mbalimbali na kuacha tabia ya kukaa maofisini, kwani
mfano unaonesha kwamba barabara hiyo viongozi walikuwa hawasimamii kwa ukaribu
ndio maana utekelezaji wake umekuwa ni wa hovyo.
Kwa upande wake alipotakiwa kutolea ufafanuzi juu ya malipo
yaliyofanyika kwa wakandarasi hao Kaimu Mhandisi wa ujenzi halmashauri ya
wilaya ya Mbinga, Said Almas alimweleza Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Mahenge
kwamba Kampuni ya Canopies International Tanzania Limited na G’S Contractors
Company Limited fedha zilizotumika kuwalipa ni jumla ya Euro 926,966.62 kati ya
fedha zilizotolewa Euro milioni 4,834,224.55 ambapo hadi mradi kukamilika kwake
zimebakia Euro milioni 3,907,257.93.
Naye Salum Mjema ambaye ni Mhandisi mshauri na mkaguzi mkuu
wa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo alikiri kuchelewa kukamilika kwa mradi huo
kwa siku walizopewa, akidai kwamba tatizo hilo limetokana na hali ya hewa mvua
kunyesha na kusababisha kazi kusimama kwa muda.
Hata hivyo baada ya kutoa maelezo hayo Dkt. Mahenge alipingana naye na kueleza kwamba, kwa kisingizio cha mvua huo ni wizi na kuficha maovu waliyoyafanya hivyo serikali itakapokamilisha uchunguzi wake na kubaini hujuma zilizofanyika wakandarasi hao watasitishiwa mikataba yao ya kazi na mitambo yao ya kufanyia kazi itakamatwa na kwamba watalazimika kurejesha fedha zote walizolipwa ili tenda ya ujenzi wa barabara hiyo, iweze kutangazwa upya na kumpata mkandarasi mwingine atakayefanya kazi kwa viwango vinavyokubalika.
No comments:
Post a Comment