Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu.
|
Na Mwandishi maalum,
Dar.
KAMATI Kuu ya CCM imepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kusikitisha
za kifo cha Mjumbe wa halmashauri kuu wa miaka mingi, msanii wa Chama Cha Mapinduzi,
kada mzoefu Kapteni John Komba.
Kwa maneno ya Mwenyekiti wa chama
hicho, alisema kifo cha Komba ni pengo lisilozibika na Chama Cha Mapinduzi
kimepata pigo kubwa, huku Komba akibaki kwenye historia
iliyotukuka.
Wasimamishwa:
Pia Kamati kuu imewasimamisha, Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu, Andrew Chenge ambaye
ni mjumbe wa Halmashauri kuu pamoja na William Ngeleja mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kuhudhuria vikao vya maamuzi vya chama kwa
kipindi ambacho kamati hii ndogo ya maadili wakiendelea na kazi yao ya kupitia baadhi ya nyaraka mbalimbali zinazohusiana na suala hili.
Akizungumzia kuhusu adhabu
walizopewa wale wanachama sita, waliojitokeza na kuanza shughuli za kampeni za
kuwania nafasi ya kuchaguliwa na chama kugombea urais alisema kamati ndogo ya
maadili inaendelea na uchunguzi wake.
No comments:
Post a Comment