Padre Baptiste Mapunda. |
Na Padre Baptiste Mapunda,
NI hivi majuzi tu, gazeti la Mwananchi liliamua kuweka mbele
ujumbe uliokuwa ukisomeka TAIFA NJIA PANDA. Kichwa hiki cha habari kilisindikizwa
na vitu vitatu vilivyo chagiza habari kuu kuwa ni mashine za BVR, Mahakama ya
Kadhi na Upigaji wa kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekezwa.
Hakika mhariri wa gazeti hili aliitendea haki, juu ya habari
iliyobeba kwenye gazeti hilo kwa kutoa habari kwa kina na kuonyesha kwa nini, taifa
lipo njia panda sasa. Leo nasi wakristo wakatoliki tunaweza kujihesabu kuwa tupo
njia panda kuhusiana na tamko la Jukwaa la kikristo Tanzania, lililotutaka
wakristo wote kuungana na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na hatimaye
kujitokeza siku ya kupiga kura ya kuipitisha katiba inayopendekezwa, kwa
kuipigia kura ya hapana.
Hii siyo kwa chuki tu, bali sababu zenye mashiko zimetolewa
na Baraza au Jukwaa hilo karibu kila aliyemkristu alizikubali sababu hizo na
kuona kwamba, zina mashiko makubwa.
Tukiwa katika hali ya umoja wa wakristo wote katika hili,
ghafla bin vuuu, Baba yetu ambaye tunamtegemea na kumwamini, Kadinali Pengo,
anajitokeza wazi kupinga sauti ya wengi ambayo sote tunaamini ni sauti ya Mungu
na kutoa maelekezo tofauti kabisa na maamuzi ya Jukwaa hili na kubaki
tunamshangaa!!. Hapa ndipo msingi wa swali langu kwenu wadau, PENGO NI KIGEUGEU
au HATAMBUI JUKWAA LA KIKRISTO TANZANIA?
Lakini pia kauli ya Pengo inatufanya sisi vijana wakikristo
tujiulize, je pengo anakemea jamii iache uovu, ukandamizaji wa haki kwa
wanyonge, mauaji ya watu wenye ulemavu na kadhalika? au ana tufundisha nini?
Hakuna asiye jua kuwa viongozi wetu sasa hawana maadili, wezi wasiojali kabisa
maisha ya wanyonge na kwa hiyo wanampango
kwa mkono wa kulia na kuchukua kwa mkono wa kushoto hivyo viongozi hawa hawana
uwezo na sifa ya kulitengenezea Taifa hili Katiba bora.
Tunajua wazi na tuliona ubabe wa Samwel Sitta na wenzake
kwenye Bunge la Katiba jambo lilotia shaka mapema kuwa hatuwezi kupata katiba
inayojali na kuzingatia maslahi ya wanyonge.
Sasa Pengo haya yote hayakumbuki? au hakuyaona na kama
hakuyaona hata kusikia hakuyasikia? Kwa nini leo hii anatugawa wakatoliki? ukweli
huku tuliko sisi wananchi wamechoka kuishi hali ya mateso, manyanyaso na
kuonewa kila wakati. Isitoshe watu wanaishi maisha magumu na wengine yasiyo
kuwa na uhakika wa kesho!! yawezekana Pengo hajui haya, msaidieni kumwambia.
Kwanza sisi tunaamini sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, Pengo
kama alishaona kanisa limeshiriki katika waraka uliotolewa na Jukwaa la
kikristo, kwa nini hakutumia busara ya kawaida tu, kukaa kimya kama alivyokaa
kimya kwenye swala Escrow ambalo maaskofu wenzake walipewa mgao pia? Mbona
hatuja wahi kumsikia akilitetea kanisa linavyopigwa mawe na madhehebu mengi
kuwa wakatoliki wezi na wanashiriki katika wizi wa fedha za umma?
Mimi niombe tu kuwa, Pengo ashauriwe kukaa kimya kwani ameshapokea
zawadi ya maisha kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu katika hali ya amani na usalama,
kwenye taifa hili; kwa hiyo na tunatamani kuishi katika amani hiyo na siyo
mikononi mwa mahakama ya kadhi inayolenga kuwafanya wakristo kuuawa na watu
wabaya na hatimaye kulimaliza kanisa.
Pengo aangalie yanayotokea Afrika ya Kati na mataifa mengine
yenye mahakama ya kazi na madhara yake kwa wakristo, hii ni hatari ambayo
inakuja mbele yetu tuwe makini katika kupembua mambo.
Lakini pia Niwatie moyo na kuwashukuru mababa wema
mliojitolea kulitetea kanisa lisitiwe mikononi mwa watu waovu. Endeleeni
kuifanya kazi ya bwana mlioitiwa bila woga wala mashaka, kwani kundi kubwa la
watu wa Mungu lipo nyuma yenu na hakika mkono wa bwana hauta waondokea. Zaidi
tunawaombeeni ili Mungu awapeni hekima katika kazi yake hii.
Niombe na nisisitize kuwa waelezeni makutano mambo haya kwa
uwazi bila kificho kwao juu ya udhaifu na imejaa hofu kuu. Lakini pia kizazaa
hiki cha leo kubambanua mambo hakiwezi, ndio maana tunasema waelezwe wazi juu
ya maamuzi ya mababa ili wajibu wao wakautimize vyema wakati ukifika. Bwana na
awabariki sana…………...
No comments:
Post a Comment