Na Nathan Mtega,
Songea.
KITUO cha hifadhi ya
taifa ya chakula (NFRA) cha Songea mkoani Ruvuma, kwa kushirikiana na kampuni
ya uhifadhi wa chakula ya AGRA kimezindua teknolojia mpya ya uhifadhi wa mazao,
ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti uharibifu wa mahindi ambayo zaidi
ya tani 78,000 yamehifadhiwa nje ya maghala, huku mengine yakiendelea kuharibika
kutokana na kituo hicho kuelemewa na wingi wa zao hilo ambayo huzalishwa na
wakulima mkoani humo.
Maghala ya kituo
hicho, yana uwezo wa kuhifadhi tani 26.000 na kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
hifadhi ya chakula taifa, Charles Warwa alisema zaidi ya tani 78.000
yameshindwa kuhifadhiwa ndani ya maghala na kulazimika kuyaweka nje, ambapo
baadhi ya magunia ya mahindi yameanza kuharibika na kuliwa na wadudu, kutokana
na teknolojia duni ya uhifadhi wa chakula unaofanywa katika kituo hicho.
Alisema hali hiyo inawafanya
wafanyakazi wa hifadhi ya chakula katika ngazi ya mikoa na taifa, kuwakosesha
usingizi lakini ujio wa teknolojia mpya ya uhifadhi wa chakula iliyoletwa na
kamuni washirika ya AGRA, itakuwa ni ufumbuzi tosha wa changamoto hiyo ambapo
kwa kituo cha Songea kuna tani zaidi ya 78,000 zimehifadhiwa nje kwa kutumia
telnolojia ya zamani, ambayo hudhoofisha ubora wa mazao na kuharibu soko la
ndani na nje.
Akizungumzia hilo,
mwakilishi wa kampuni hiyo ya AGRA Tanzania, Dokta Mary Mgonja alisema kampuni
hiyo imekuja na teknolojia mpya ya kunusuru uharibifu huo kwa kutumia uhifadhi
wa kisasa wa chakula, wakianzia ngazi ya jamii hadi hifadhi ya chakula ya taifa
ambao hauna gharama ya kutumia madawa, ambayo wakulima wengi wamekuwa
wakishindwa kumudu kuyanunua na kujikuta mazao yao yakiishia kuharibika.
Baadhi ya wakulima wa
mahindi wilayani Songea mkoani Ruvuma, pamoja na kuonesha wasi wasi wa mbinu
hiyo ya uhifadhi wa chakula lakini wamepongeza kampuni hiyo kwa kuja na njia
mbadala ya uhifadhi wa mazao yao, ambayo haina gharama kubwa na itapunguza
uharibifu wa mazao huku mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu akisema mpango
huo ni mzuri na umekuja wakati muafaka kwa sababu uzalishaji wa mazao
yanayohitaji uhifadhi huo, yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa.
No comments:
Post a Comment