Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu akisisitiza jambo katika kikao hicho mjini Tunduru mkoani humo. |
Na Steven Augustino,
Tunduru.
MKUU wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amewataka Wakuu wa wilaya
na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa huo, kuamka kutoka usingizini na kuanza
kazi ya kukabiliana na changamoto ya utoro na mdondoko mkubwa wa wananfunzi
ambao wamekuwa hawaendelei ipasavyo na masomo, katika shule za msingi na sekondari.
Mwambugu alitoa agizo hilo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa
Wadau wa tathimini ya elimu mkoni Ruvuma, uliofanyika kwenye ukumbi wa Klasta ya walimu tarafa ya
mlingoti mjini Tunduru na kuhakikisha watoto wote wanaoandikishwa, wanamaliza
elimu ya msingi na kundelea na masomo ya sekondari.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, takwimu zinaonesha kuwa mkoa huo
unakabiliwa na mdondoko wa kutisha ambapo mwaka 2008 ulindikisha wanafunzi wa
darasa la kwanza 41,789 lakini takwimu za wanafunzi waliofanya mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi, mwaka 2014 walikuwa 27,771 sawa na asilimia 66.
Alisema kwa mujibu takwimu hizo watoto 14,018 walipotea mitaani
hawakuhudhuria masomo, hali ambayo alisema kwamba haivumiliki na kuendelea kufumbiwa
macho na kuacha vijana hao ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hili, wakiangamia kwa kukosa maarifa.
Kufuatia hali hiyo, Mwambungu aliwataka viongozi hkatika mkoa huo
kujenga ushirikiano kutoka ngazi ya kitongoji, kijiji, mtaa na kata kwa
kuchukua majukumu ya kuhakikisha watoto wote walioandikishwa wanahudhuria
masomo darasani kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
Alisema endapo kutakuwa na kikwazo cha aina yoyote ile kutoka kwa
mzazi husika, ni wakati wa kuwafikisha mahakamani ili hatua stahiki zichukuliwe
na kuondokana na tabaka la watoto ambao hawataki kwenda shule.
Katika kuhakikisha kwamba mkoa huo, unasonga mbele kitaaluma maafisa
elimu wameagizwa waliopo ndani ya mkoa wanapanga utaratibu kuwa, walimu katika
shule zote wanapaswa kufanya kazi katika eneo lolote, yakiwemo maeneo ya shule
zilizopo vijijini.
Akitoa taarifa ya hali ya elimu mkoani humo, Afisa elimu wa mkoa
wa Ruvuma Mayasa Hashim alisema pamoja na kuwepo kwa upungufu wa miundo mbinu
kwa mwaka 2014 mkoa huo, uliweza kufaulisha jumla ya wanafunzi 15,209 na kuongeza idadi ya ufaulu wa
asilimia 16 baada ya kufikia asilimia 54 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka
2013.
Idadi hiyo inatokana na mkoa kusajili watahiniwa 28,418 ambapo
kati yao wanafunzi 27,711 walifanya mtihani huo na kwamba mchanganuo unaonesha kuwa kati
ya watoto hao waliofaulu, watoto 116
walichaguliwa kwenda kujiunga katika shule maalumu na wengine waliobakia
walipelekwa kwenda kujiunga na masomo ya sekondari, katika shule zilizopo zilizopo
hapa mkoani Ruvuma.
Hashimu alifafanua kuwa ingawa ufaulu huo ni mdogo, na ambao
umeufanya mkoa huo kutofikia lengo la matokeo makubwa sasa (BRN) la asilimia 66
na kwamba ili kufikia lengo hilo, mkoa wake umejipanga kuhakikisha kwamba wanalifikia
katika matokeo ya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment