Na Kassian Nyandindi,
Songea.
DOKTA John Pombe Magufuli, ambaye ni mgombea Urais kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini anatarajiwa kupokelewa na
maelfu ya wananchi na wapenzi chama hicho, katika kijiji cha Igawisenga
wilayani Songea mkoani humo akitokea mkoa wa Njombe tayari kwa kuanza kampeni ya
chama hicho ndani ya mkoa huo.
Waandishi wa habari waliozungumza na Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya kampeni ya CCM hapa Ruvuma, Ramadhan Kayombo alisema kuwa Dokta
Magufuli na msafara wake unatarajiwa kupokelewa Agosti 30 mwaka huu, majira ya
asubuhi katika kijiji hicho.
Kayombo alisema Chama hicho, kimejipanga kikamilifu katika
kuhakikisha kwamba mgombea huyo, wabunge na madiwani ndani ya mkoa huo wanafanyiwa
kampeni zenye ustaarabu na sio vinginevyo.
Dokta Magufuli anatarajia kufanya ziara yake ya kampeni mkoani
Ruvuma katika wilaya ya Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru ambako
atamaliza ziara yake Septemba 2 mwaka huu na kuendelea mkoani Mtwara.
Mwenyekiti huyo wa maandalizi ya kampeni ya CCM mkoani humo,
alifafanua kuwa wananchi wengi wanaimani na chama hicho na kwamba wanahitaji
kumuona mgombea huyo na kumsikiliza sera zake.
Alisema kwa kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye
mikutano ya hadhara, itakayofanyika wakati Dokta Magufuli atakapokuwa amewasili
hapa mkoani Ruvuma huku akiwaomba kuwa na mshikamano wa pamoja katika
kuhakikisha CCM kwenye uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka
huu kinapata ushindi wa kishindo kwa mgombea nafasi ya urais, wabunge na madiwani.
No comments:
Post a Comment