Sunday, October 9, 2016

BENKI YA NMB TAWI LA LITEMBO MBINGA YAMWAGA MISAADA HOSPITALI YA MISHENI LITEMBO

 Kaimu Mganga mkuu hospitali ya Misheni Litembo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la  Mbinga mkoani Ruvuma, Dkt. Maurus Ndomba upande wa kushoto, akipokea sehemu ya shuka 46 kutoka kwa Meneja wa benki ya NMB tawi la Litembo Kennedy Chinguile, ili zisaidie wagonjwa katika hospitali hiyo, katikati ni katibu wa afya wa hospitali hiyo, Anna Mwenda.
 Katibu wa hospitali ya Misheni Litembo, Anna Mwenda upande wa kulia akizungumza  jambo kabla ya kupokea msaada wa shuka 46 kutoka kwa uongozi wa benki ya NMB tawi la Litembo wilayani Mbinga mkoani hapa, wa pili upande wa kulia ni Meneja wa NMB tawi la Litembo, Kennedy Chinguile na wa tatu ni Kaimu Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Maurus Ndomba.
 Katibu wa hospitali ya Misheni Litembo wilayani Mbinga, Anna Mwenda upande wa kulia akimshukuru mmoja kati ya wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Litembo mara baada ya kupokea msaada wa shuka 46 kwa ajili ya matumizi katika hospitali hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Litembo wilayani Mbinga wakitoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Misheni Litembo wilayani humo.
 Mmoja kati ya wagonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Misheni Litembo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, Folkwati Komba(4) akimsalimia kwa mkono wake mfanyakazi wa benki ya NMB ambaye hakufahamika jina lake mara moja, baada ya benki hiyo kutoa msaada wa mashuka na vitu mbalimbali.
 Wafanyakazi wa NMB tawi la Litembo, wakitoa msaada kwa mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Misheni Litembo wilayani Mbinga.
 Meneja wa benki ya NMB tawi la Litembo wilaya ya Mbinga, Kennedy Chinguile akitoa pole kwa mtoto Folkwati Komba aliyelazwa katika hospitali ya Misheni Litembo wilayani humo.
 Meneja wa benki ya NMB tawi la Litembo wilaya ya Mbinga, Kennedy Chinguile akimfariji mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Misheni Litembo wilayani hapa.
Katibu wa hospitali ya Misheni Litembo wilayani Mbinga, Anna Mwenda upande wa kulia akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Litembo mara baada ya kupokea msaada wa shuka 46 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo. (Picha zote na Muhidin Amri)

No comments: