Uharibifu namna unavyoendelea. |
WANANCHI waishio katika tarafa ya Wanging'ombe mkoani Njombe
wapo hatarini kukumbwa na baa la njaa, kufuatia eneo la tarafa hiyo kukosa mvua
kwa muda mrefu na mazao yao kushindwa kuendelea kustawi kutokana na uharibifu
wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.
Hayo yamebainika kufuatia kikosi kazi kilichoundwa na Makamu
wa Rais, Samia Suluhu Hassan kutembelea katika eneo hilo na kushuhudia
uharibifu uliofanyika.
Ofisa kilimo wa wilaya hiyo Bernadeta Fivao alisema kuwa
licha ya serikali kuzuia wananchi kulima kwenye vyanzo vya maji, kumekuwa na
baadhi ya wakulima katika tarafa hiyo wakiendelea kulima kwenye vyanzo vya maji
kutokana na kukosa chakula.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya Wangingombe wameeleza
wakidai kuwa Madiwani na Wabunge ndiyo wamekuwa wakihamasisha wananchi
kuendelea kuharibu vyanzo hivyo vya maji.
Hivi sasa eneo la tarafa ya Wangingombe limekuwa likikabiliwa
na tatizo kubwa la uhaba wa maji kutokana pia na kuwepo wa vitendo vya ufugaji
holela pamoja uharibifu wa vyanzo hivyo kwa kuendesha kilimo cha mazao kando kando
ya mito.
No comments:
Post a Comment