Na Mwandishi wetu,
Mbinga.
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mbinga mkoa wa
Ruvuma, wamemchagua Joackimu Kowelo ambaye ni diwani wa kata ya Maguu kuwa
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Uchaguzi huo ulifanyika jana majira ya asubuhi katika ukumbi
wa CCM uliopo mjini hapa.
Katibu wa Chama hicho wilayani humo, Zainabu Chinowa ambaye
alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, akitangaza matokeo hayo alimtaja Kowelo
kuwa ndiye aliyeweza kushinda katika uchaguzi huo kwa kupata kura 26 dhidi ya
mgombea mwenzake diwani wa kata ya Matiri, Benuward Komba aliyepata kura 7.
“Ndugu zangu uchaguzi umeenda vizuri tumeufanya kwa usalama
na amani, wapiga kura walikuwa 34 kati ya hawa kura moja tu ndiyo iliyoharibika
nadhani ni bahati mbaya ambayo inaonesha mpiga kura hakuwa na msimamo mzuri”,
alisema Chinowa.
Hata hivyo pamoja na mambo mengine, chaguzi za kumchagua
makamu Mwenyekiti wa kuongoza halmashauri ya wilaya zimekuwa zikifanyika kila
baada ya mwaka mmoja na kwamba awali halmashauri ya wilaya ya Mbinga katika
nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na diwani wa kata ya Matiri, Benuward Komba.
No comments:
Post a Comment