Baadhi ya aina ya vipodozi ambavyo vinadaiwa kuwa na sumu vilivyokamatwa Songea. |
Na Mwandishi wetu,
Songea.
IDARA ya Afya katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,
imefanikiwa kukamata vipodozi na vyakula vyenye sumu vikiwa na thamani ya zaidi
ya shilingi milioni mbili.
Afisa habari wa Manispaa hiyo, Albano Midelo alisema kuwa vipodozi
hivyo vimekamatwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu,
katika ukaguzi endelevu ambao unafanywa na idara hiyo.
Vipodozi vyenye sumu ambavyo vimekamatwa baadhi yake ni Actif
plus, Betasol, Broze, Cocoderm, Carolight, Carotone, Citrolight, Clairmen, Cocopulp,
Corton, Diproson na Epiderm.
Aidha vingine ni Extralair, Jaribu, Lemonvate na Mekako, Miki,
Montclair, Movate, Naomi, Oranvategel, Perfect, Princes, Rapid, Sabuni protex,
Seven mirackes, Toplemon, Whiteplus, Dodo, Teint, Superclair, Greeting, 14 days,
Dermotyl, Natural, Gold touch, Coco dermbetacort, Extral white, Fomura avas, Lemon
cream na Diva maxmum.
Midelo alisema kuwa katika ukaguzi huo pia vimenaswa vipodozi
halali ambavyo vimemalizika muda wake wa matumizi navyo vina thamani ya shilingi
500,000 na kwamba vimetajwa kuwa ni Soft, Pure glycerine, Royal touch, U & me
na Mambo fresh.
Katika kipindi hicho idara hiyo ya afya katika Manispaa ya
Songea imekamata pia vyakula vilivyokuwa vinauzwa wakati muda wake umekwisha navyo
vina thamani ya shilingi 300,000.
No comments:
Post a Comment