Tuesday, July 7, 2015

POLISI WAMSAKA BINTI ALIYETUPA KICHANGA CHOONI

Na Steven Augustino,
Songea.   

JESHI la Polisi wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wanamtafuta binti mwenye umri wa miaka 19 kwa lengo la kutaka kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, ili aweze kujibu tuhuma za mauaji ya kichanga na mwili wake kuutumbukiza chooni.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela alisema kuwa mtuhumiwa huyo alifanya unyama huo juzi na kutokomea kusikojulikana.

Msikhela alimtaja mtuhumiwa aliyefanya kitendo hicho kuwa ni, Germana Ndimbo mkazi wa kijiji cha Mkumbi kata ya Mkumbi wilayani humo ambapo alikuwa mjamzito na mara alipofanikiwa kujifungua, alichukua jukumu la kufanya unyama huo.


Alifafanua kuwa kichanga hicho alikitumbukiza katika choo cha nyumba ya Damas Komba ambaye ni jirani yake.

Tukio hilo liligunduliwa na Komba mara baada ya kuingia chooni na kukuta mikwaruzo katika shimo la choo chake, na kwamba alipoangalia alibaini uwepo wa mwili wa kichanga hicho.

Baada ya kuona hilo, ndipo alichukua jukumu la kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali ya kijiji hicho ambapo walishirikiana na wananchi wa mtaa huo, kubomoa shimo hilo la choo na kukuta mwili wa kichanga, hatimaye waliliripoti kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Mbinga kwa uchunguzi zaidi.

No comments: