Saturday, July 26, 2014

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AMTAKA MKAGUZI WA NDANI HALMASHAURI YA MBINGA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE YA KAZI BILA KUINGILIWA

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu (watatu kutoka kushoto) nje ya ukumbi wa jumba la maendeleo uliopo mjini hapa.
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amemuagiza Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani humo kuhakikisha kwamba, anatoa taarifa sahihi na kwa wakati juu ya mwenendo wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi wilayani humo ili kuepukana na malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

Sambamba na hilo aliwataka watendaji husika katika halmashauri hiyo kutoingilia utendaji kazi wa ofisi ya mkaguzi huyo, huku akisema kuwa ni ofisi ambayo ipo huru na inafanya kazi zake bila kuingiliwa na mtu yeyote.

"Sasa hivi ndugu zangu nahitaji mtambue kuwa ofisi ya mkaguzi wa ndani katika halmashauri ni idara kamilifu ambayo ipo huru, kwa hiyo ninachosema hapa mkaguzi fanya kazi zako bila kuingiliwa na mtu wewe una jukumu kubwa sana", alisema Mwambungu.

Mwambungu alitoa rai hiyo alipokuwa akihutubia leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya Mbinga, lililofanyika kwenye ukumbi wa jumba la Maendeleo uliopo mjini hapa.

Tuesday, July 22, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AWA MBOGO, AMUAGIZA MKUU WA MKOA WA RUVUMA KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WALIOHUSIKA NA WIZI WA FEDHA ZA WAKULIMA

Na Kassian Nyandindi,

Namtumbo.

RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu ahakikishe kwamba anawakamata na kuwafikisha Mahakamani wale wote ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine, kufanya ubadhirifu wa fedha za wakulima wa tumbaku wilaya ya Songea na Namtumbo mkoani humo.

Aidha agizo hilo limefuatia baada ya Mwambungu kuunda tume ya kuchunguza tatizo hilo, ambayo inaendelea kufanya kazi ya ukaguzi wa hesabu za fedha kwa chama cha ushirika wa wakulima wanaozalisha zao hilo kutoka kwenye wilaya hizo mbili (SONAMCU).

Kikwete ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho na kufikia hatua ya kutoa agizo hilo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa, katika mkutano wa hadhara wa wananchi uliofanyika mjini hapa.

HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO

Na Kassian Nyandindi,
Songea.

RAIS  Dokta Jakaya Kikwete ameziagiza Halmashauri za wilaya na Manispaa hapa nchini, kuongeza vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea wafadhili na serikali kuu.

Akihutubia mkutano wa hadhara mara baada ya kufungua soko la kimataifa la Mkenda ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 169 na ambalo lipo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, wilaya ya Songea mkoani Ruvuma alisema viongozi na watendaji wasipokuwa wabunifu katika kuongeza vyanzo vipya vya mapato hawataweza kusonga mbele kimaendeleo.

Kikwete alisema halmashauri nyingi zimekuwa zikitegemea chanzo kimoja cha mapato, hususan fedha zinazotolewa na serikali kuu jambo ambalo husababisha utekelezaji wa baadhi ya miradi ya wananchi kukwama.

Monday, July 21, 2014

ROAD CONSTRUCTED AT TARMAC LEVEL AND FUND MILLENNIUM CHALLENGES TO MBINGA PERAMIHO LAUNCHED

President of the United Republic of Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete, making the launch of the road was built at a rate of tar from Peramiho junction to Mbinga. The launch took place in the area of ​​urban Mbinga being accompanied by other officials including the ambassador of the People's Republic of China in the country, Dr. Lu Youqing.
By Kassian Nyandindi,

Ruvuma.

CONSTRUCTION of a road mile 78 at a rate of tar from the Peramiho junction Songea District villages to Mbinga Ruvuma Region, has been officially launched by the President of the United Republic of Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete, with its construction waste has cost more than Tshs 100 million, including the cost of management.

That's one of the dollars raised USD 64.3 times last in the administration of former President George Bush, as part of the support for creating various development projects in the country.

Initially he read reports of the Chairman of the board of the fund to the challenges of the millennium Tanzania (MCAT) prior to the exercise of the launch of the road in front of the president, Engineer Patric Mfugale said that the company Sinohydro Corporation Limited from China is that handed the task of construction of paved rate from Songea to Mbinga, and that its construction until completion has taken 39 months.

MBINGA YA KWANZA KITAIFA KUFANYA VIZURI KIELIMU


Na Kassian Nyandindi,

Ruvuma.

NAIBU Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Jenister Mhagama ameipongeza wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kuwa ya kwanza kitaifa kufanya vizuri kielimu kwa shule za msingi, katika maendeleo ya mpango wa kipimo cha matokeo makubwa hapa nchini (BRN).

Mhagama alitoa pongezi hizo wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa mji wa Mbinga, na kusema kuwa matokeo hayo yametokana na viongozi wa wilaya hiyo kushirikiana ipasavyo na walimu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

“Wilaya hii ya Mbinga imekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kuboresha maendeleo kwenye sekta ya elimu, nawapongeza sana nawaomba endelezeni jitihada hizi kwa faida ya kizazi chetu cha sasa na baadae”, alisema Mhagama.

KITUO CHA KISASA MABASI YA ABIRIA MBINGA CHAFUNGULIWA, RAIS APONGEZA UONGOZI WA WILAYA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete, akifungua kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria Mbinga mjini mkoani Ruvuma.
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Kikwete hatimaye amefanya ufunguzi wa kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria ambacho kimejengwa Mbinga mjini mkoa wa Ruvuma, kwa thamani ya shilingi bilioni 2.1.

Fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana na mkopo kutoka bodi ya mikopo ya serikali za mitaa, ambapo majengo pacha ya ghorofa moja yamejengwa yakiwa na vyumba 112 vya kufanyia biashara.

Aidha majengo hayo yana sehemu ya kupumzika abiria, kuegesha magari, miundombinu ya usafi, maji na ya tahadhari ya moto ambapo ujenzi wake umechukua muda wa miezi 39.

Saturday, July 19, 2014

RAIS KIKWETE AWATAKA WAKULIMA WA KAHAWA KUWA NA NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA

Rais Jakaya Kikwete akiangalia vikundi vya ngoma katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Mbinga, mara baada ya kuwasili akitokea wilaya ya Nyasa. Upande wa kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Senyi Ngaga.

 Rais Jakaya Kikwete upande wa kulia akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Mbinga, John Ndimbo mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo. (Picha zote na Kassian Nyandindi)
Na Kassian Nyandindi,


Mbinga.  

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amewataka wakulima wanaozalisha zao la kahawa wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, kutumia fedha walizokopeshwa na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) kwa makusudio yaliyowekwa na sio vinginevyo.

Kikwete alisema hayo baada ya kukabidhi hundi ya shilingi bilioni 2 kwa vyama vinne vya ushirika ambavyo hujishughulisha na uzalishaji wa zao hilo wilayani humo, ambavyo kila kimoja vimekopeshwa shilingi milioni 500.

Aliwataka viongozi na wanachama wa ushirika husika, kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha hizo ili waweze kurejesha kwa wakati na wanachama waweze kunufaika na mkopo huo.

MAMA SALMA KIKWETE AWAPA SOMO AKINA MAMA MBINGA


Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

VIFO vinayotokana na akina mama wajawazito wakati wa kujifungua hapa nchini, vimepungua kutoka akina mama 578 miaka ya nyuma na kufikia 454 mwaka huu kati ya vizazi hai 100,000 ambao walikuwa wakijifungulia nyumbani na kusababisha mtoto au mama kufariki dunia.

Upungufu huo umetokana na jitihada ya serikali kufanya kazi ya ujenzi wa zahanati vijijini na vituo vya afya kwa kila kata, ambapo akina mama wengi wajawazito huenda huko kwa ajili ya kupata huduma husika tofauti na kujifungulia majumbani.

Hayo yalisemwa leo na mke wa Rais hapa nchini, Mama Salma Kikwete alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Mama Salma alisema ujenzi wa vituo hivyo vya kutolea huduma za afya vijijini ulilenga kupunguza tatizo hilo, na kwamba ni ahadi iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi na ambayo ipo katika ilani yake.

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAKULIMA SOKO LA MAHINDI, JK ASEMA SHILINGI BILIONI 15 ZIMETENGWA KUNUNULIA ZAO HILO


Na Kassian Nyandindi,
Songea.

RAIS Jakaya Kikwete amesema serikali imetenga shilingi bilioni 15 zikazotumika kununulia mazao ya wakulima, kupitia wakala wa hifadhi ya chakula ya taifa nchini(NFRA) kuanzia Agosti mosi mwaka huu msimu wa mavuno ya zao la mahindi utakapofunguliwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kuzindua ghala jipya la hifadhi ya taifa ya chakula, lililopo eneo la Ruhuwiko mjini Songea alisema kuwa ili kuweza kuhifadhi mazao mengi kwa wakati mmoja ni lazima pawe na maghala mengi na ya kisasa.

Alisema hivi sasa taifa lina akiba ya kutosha ya chakula ambapo maghala yake yamejaa mazao, ikiwemo ghala la NFRA la mjini hapa ambapo kuna tani 51,000 ambazo bado hazijaondolewa huku wakati wa kununua mazao mapya ukiwa umewadia.

BALOZI WA CHINA AMPONGEZA RAIS KIKWETE


Na Dustan Ndunguru,
Mbinga.

BALOZI wa China nchini Lu Youqing amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete kutokana na kazi yake kubwa, anayoifanya ya kusimamia shughuli za ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami jambo ambalo litasaidia kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.

Pongezi hizo alizitoa wakati alipokuwa akiongea katika mkutano wa hadhara mjini hapa, mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Peramiho yenye urefu wa kilometa 78 ambayo imejengwa na kampuni ya SINOHYDRO ya nchini China.

Lu Youqing alisema kuwa watanzania wanapaswa kuendelea kuunga jitihada zinazofanywa na serikali yao, ili waweze kuondokana na umasikini wa kipato na kwamba serikali ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Friday, July 18, 2014

KIUNGI MKOMBOZI KWA WANAWAKE MBINGA KATIKA KUMILIKI ARDHI

Mama mmoja ambaye ni Ostina Msuha mkazi wa kijiji cha Ndembo kata ya Linda akiwa katika eneo la ardhi yake yenye zaidi ya ekari mbili kijijini hapo, ambapo iliporwa na hatimaye akafanya jitihada ya kupigania kwa kufuata sheria husika na kufanikiwa kuirejesha mikononi mwake baada ya kupewa elimu na umoja wa kikundi cha maendeleo ya wanawake (KIUNGI) juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi.

Adelehema Nombo mkazi wa kijiji cha Lituru kata ya Litembo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma akitoa ushuhuda wa eneo la ardhi yake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) ambayo imeporwa na wajanja wachache kwa muda wa miaka minne na kuuziwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Samwel Jaboma mkazi wa Litembo, hivyo baada ya kupewa elimu juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi ameanza jitihada ya kupigania haki yake kwa lengo la kuirejesha mikononi mwake. (Picha zote na Kassian Nyandindi)
Na Kassian Nyandindi,


Mbinga.

IMEELEZWA kuwa asilimia 95 ya ardhi wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, inamilikiwa na wanaume wakati asilimia tano tu ndio humiliki wanawake wachache huku mila na desturi zikiwakandamiza wanawake na kuwanyima fursa, ya kumiliki rasilimali hiyo muhimu.

Sambamba na hilo wanawake sita kati ya 10 wilayani humo ndio ambao huporwa ardhi za mashamba yao na ndugu wa marehemu baada ya kufiwa na mume, hivyo katika kuondokana na tatizo hilo jitihada za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kuweza kuondokana na hali hiyo.

Kufuatia hali hiyo, umoja wa kikundi cha maendeleo ya wanawake (KIUNGI) wilayani Mbinga umeweza kutambua matatizo hayo yanayowakabili wanawake wilayani humo, katika dhana nzima ya umiliki wa rasilimali ardhi na kuanza kutoa elimu juu ya haki za kundi hilo kumiliki ardhi.

Thursday, July 17, 2014

UZINDUZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU SONGEA WAFANA, RAIS AIPONGEZA NHC


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu (upande wa kulia), Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) David Shambwe wakikata utepe kwa pamoja ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa nyumba za shirika hilo.
 Rais Kikwete akipata taarifa ya mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC mjini Songea, kutoka kwa kaimu mkurugenzi wa shirika hilo  David Shambwe.
 
  Rais Kikwete akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa nyumba mjini Songea, ambapo aliipongeza NHC kwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na kulitaka shirika hilo liendeleze jitihada hizo za ujenzi wa nyumba bora.
 
 Rais Kikwete akipata maelezo juu ya Mashine za kufyatulia matofali  ambazo zimegawiwa kwa kila wilaya za mkoa wa  Ruvuma.
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika hafla hiyo mchana wa leo mjini Songea.
 
 Akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo la ufunguzi wa nyumba hizo.

Vikundi mbalimbali vya ngoma za asili mkoani Ruvuma, vikitoa burudani wakati Rais Kikwete akiwasili eneo la tukio la ufunguzi wa nyumba hizo. (Picha zote kwa hisani ya NHC)
 

KITUO CHA POLISI TUNDURU CHAVAMIWA NA KUVURUGWA



Na Mwandishi wetu,
Songea.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linaendesha msako mkali katika kijiji cha Lukumbule wilayani Tunduru mkoani humo, kwa lengo la kuwapata wahuni waliovamia kituo cha Polisi kung’oa bati, kuiba sola na kuchoma pikipiki ya askari wa usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Mihayo Msikela akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa alisema tukio hilo lilitokea Julai 11 mwaka huu, majira ya asubuhi wakati askari wa usalama barabarani mwenye namba H 925  Benjamini, akiwa na askari mwenye namba G 1921 Charles walipomsimamisha Sijaona Ally ambaye hakutii amri hiyo badala yake kumgonga askari wa usalama barabarani.
Kamanda Msikela amesema kutokana na wote wawili kupata majeraha walikimbizwa hospitali ya Lukumbule kwa matibabu zaidi.

DOKTA KIKWETE LEO AANZA ZIARA MKOANI RUVUMA, AZINDUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU SONGEA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Mkuzo, Songea mkoani Ruvuma. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa ardhi nyumba na makazi Prof. Anna Tibaijuka, Kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba la taifa David Misonge Shambwe na upande wa kulia ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu.

Ris Dokta Jakaya Kikwete akifunua jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba zilizojengwa kwa gharama nafuu na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) huko Mkuzo Songea mjini mkoani Ruvuma leo. Kushoto ni kaimu Mkurugenzi wa NHC David Misonge Shambwe na wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa ardhi nyumba na makazi Prof. Anna Tibaijuka. (Picha zote na Freddy Maro.)

Wednesday, July 16, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE KUFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI RUVUMA, WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Kikwete.

















Na Kassian Nyandindi,

Ruvuma.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atafanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ikiwemo kukagua, kufanya uzinduzi na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya Wananchi mkoani humo. 

Ziara hiyo ni ya muda wa siku saba anatarajia kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Songea Julai 17 mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi na kupokelewa na uongozi wa mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ametoa taarifa hiyo leo kwa vyombo mbalimbali vya habari, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa kwenye ukumbi wa Maliasili wa mkoa huo.

Mwambungu amewataka wananchi waliopo katika maeneo mbalimbali mkoani humo, ambako Rais Kikwete atapita kufanya shughuli hizo muhimu ikiwemo mikutano ya hadhara katika kila wilaya zilizopo hapa mkoani Ruvuma, kujitokeza kwa wingi.

Wednesday, July 9, 2014

TCDC YAWATAKA WAHUDUMU WA AFYA KUHAMASISHA JAMII KUZINGATIA MASUALA YA AFYA

Aliyesimama ni mtendaji wa kata ya Kihagara wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, Emmanuely Nkaleka akisisitiza jambo katika mafunzo ya siku mbili ya Wahudumu wa afya watendaji wa vijiji, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Jumba la maendeleo Mbinga mjini.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi wa mafunzo hayo. (Picha zote na Kassian Nyandindi)

Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

IMESISITIZWA kuwa mama mjamzito anatakiwa kwenda kliniki mapema mara baada ya kujitambua kuwa ni mjamzito, ili aweze kujifungua salama na kuepukana na madhara yanayoweza kutokea baadae.

Aidha katika kuleta ufanisi Wahudumu wa afya wilaya ya Mbinga na Nyasa mkoani Ruvuma, wametakiwa kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa utekelezaji wa jambo hilo kwa lengo la kuachana na vitendo vya akina mama wajawazito kujifungulia majumbani, badala yake waende kwenye vituo vya afya, zahanati au hospitali.

Rai hiyo ilitolewa leo na Mratibu wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, Alphonce Njawa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wahudumu wa afya watendaji wa vijiji wa wilaya hizo, ambayo yamendaliwa na shirika lisilo la kiserikali ‘Tanzania Communication and Development Center’ (TCDC) yaliyofanyika katika ukumbi wa Jumba la maendeleo mjini hapa.

Njawa alisema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwapa taarifa za mabadiliko ya kiutendaji na ongezeko la maeneo ya kufanyia kazi, pamoja na kutoa elimu ya afya kwenye jamii kuepukana na tabia hiyo na hatimaye hata kupunguza vifo visivyo vya lazima.

Monday, July 7, 2014

WANANCHI MKOANI RUVUMA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Rachel Stephen Kassanda akihutubia wananchi mbele ya Jengo la makaazi ya idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma, mara baada ya kulizindua katika kata ya  Mahenge Manispaa ya Songea. Amesema wapo wananchi wa mkoa wa  Ruvuma wanaoshirikiana na Wahamiaji haramu kuwasafirisha na kuwahifadhi katika maeneo maalumu  amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa idara hiyo ili kutokomeza vitendo hivyo.

Kiongozi mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Stephen Kassanda amesema wahamiaji walio wengi hutoka Eretria, Somalia hupitia mipaka ya mkoa wa Ruvuma.
Pichani anayehutubia ni kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014, anayefuatia katikati ni Afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza na wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti.

 Watumishi wa idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenge wa Uhuru katika jengo la makaazi la Afisa uhamiaji mjini Songea, lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Stephen Kassanda. Pichani aliye katikati ya viongozi wa mbio za Mwenge ni afisa uhamiaji wa mkoa huo Kokwi Lwebandiza.
Watumishi wa idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za Mwenge mara baada ya kuzindua jengo lao.
Mwenge wa Uhuru 2014 ukiwa na viongozi wa msafara wa mbio za Mwenge mkoani Ruvuma katika eneo la mradi wa jengo la makaazi ya uhamiaji, Mahenge Manispaa ya Songea. Wenye sare za kitenge ni kikundi cha kwaya kutoka wilaya ya Namtumbo.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa aliyeshika taarifa akiwa katika msafara wa mbio za Mwenge Manispaa ya Songea kushiriki katika uzinduzi wa miradi iliyokamilika katika halmashauri yake.
 Katika utunzaji wa mazingira mkoa wa Ruvuma, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Rachel Kassanda aliweza kupanda mti wa mkungu akiashiria kushiriki katika utunzaji wa mazingira.
 
 Afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akipokea Mwenge wa Uhuru ikiwa ni ishara ya uzalendo nchini Tanzania.
Baadhji ya maafisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda. kushoto ni Shaban, mmoja kati ya watumishi wa idara ya uhamiaji mkoani Ruvuma.

Hili ni jengo la uhamiaji mkoa wa Ruvuma lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, kitaifa lililogharimu kiasi cha shilingi 434,100,170. Lililopo Mahenge Manispaa ya Songea.


Pichani wa pili kutoka kulia afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza, akiwa na watumishi wa idara hiyo muda mfupi kabla ya msafara wa mbio za Mwenge wa Uhuru, kuwasili katika eneo la jengo la uhamiaji tayari kwa kuzindua.

Mhasibu idara ya uhamiaji mkoani Ruvuma, aliyeshika Mwenge katika eneo la jengo la makaazi ya uhamiaji mjini Songea. (Picha zote na Mwandishi wetu)

KUNDI LA SIMBA LADAIWA KUVAMIA MIFUGO YA WANANCHI NAMTUMBO


Na Steven Augustino,
Namtumbo.

KUNDI kubwa la Simba limeripotiwa kuvamia na kuanza kuua ng’ombe wa wafugaji katika vijiji vilivyopo kata ya Lusewa wilayani Namtumbo mkoani  Ruvuma,  hali ambayo imewafanya wamiliki wa mifugo hiyo kuishi kwa wasi wasi.

Awali wanakijiji hao walikuwa wakidhani kwamba mifungo yao kuwa ni wezi ndio wanaoiba, kutokana na kutojua ni nani anayehusika na upotevu wa mifugo yao.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji wakata ya Lusewa Abdallah Maniamba wakati alipokuwa akizungumza waandishi wa habari juu ya matukio hayo na kuongeza kuwa,  hali hiyo inatokana na ofisi yake kupokea taarifa kutoka  kwa mwananchi  mmoja  aliyejitambulisha kwa jina la Habari  Jamwana kuwa hivi sasa kuna kundi kubwa la simba waliovamia katika maeneo yao na wanamaliza mifugo.

Maniamba alifafanua kuwa aliwaona simba watatu dume, jike na mtoto wakinywa  maji katika  mto  chimalilo wakati  akiwa anaoga maji.

TUNDURU KUPATA HATI CHAFU KUTOKANA NA KUTOTEKELEZA IPASAVYO MIRADI YA MAENDELEO YA WANANCHI


Na Steven Augustino,
Tunduru.

HALMASHAURI ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma huenda ikapata hati chafu katika mwaka huu wa fedha, kutokana na halmashauri hiyo kutotekeleza ipasavyo ujenzi wa miradi 16 ya maendeleo ya wananchi kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 yenye thamani ya shilingi milioni 284.3.  

Mwakilishi wa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali mkoani Ruvuma, Leonard Chama alisema kuwa tatizo hilo linatokana na halmashauri hiyo kushindwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa zahanati, madarasa, visima vya maji na ofisi ya kata.

Kufuatia hali hiyo Baraza la madiwani la halmashauri hiyo limesikitishwa na hali hiyo na kuutaka uongozi husika wa wilaya ya Tunduru kuhakikisha kwamba makosa hayo hayajirudii tena.

Saturday, July 5, 2014

TAKUKURU YALIA NA VITENDO VYA RUSHWA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Aliyevaa traki suti yenye rangi ya bluu, ni Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Mbinga Ditram Mhoma, akiteta jambo na watu ambao walikuwa wakiwasili katika banda la taasisi hiyo kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru kata ya Maguu wilayani humo, kwa ajili ya kupata elimu namna ya kupambana na vitendo vya rushwa.

Baadhi ya wadau wa kupambana na rushwa wakiwa ndani ya banda la TAKUKURU katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru kata ya Maguu wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wakipewa elimu na mmoja kati ya makamanda wa takukuru wa wilaya hiyo aliyekuwa upande wa kulia, namna ya kupambana na vitendo vya rushwa. (Picha na Kassian Nyandindi)


Na Kassian Nyandindi,

Mbinga.

TAASISI ya Kuzuia, Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma imesema, wilaya hiyo inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na vitendo vya rushwa katika miradi ya maendeleo ya wananchi ikiwemo ujenzi wa majengo ya shule, barabara na miradi mbalimbali ya kilimo.

Aidha rushwa kubwa imetawala hasa kwenye kitengo cha manunuzi, ambapo jitihada zinaendelea kufanyika kuchunguza matatizo husika yaliyopo na tayari baadhi ya vigogo wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga wamefikishwa Mahakamani kujibu makosa yanayowakabili.

Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya hiyo Ditram Mhoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari, ambao walitembelea banda la taasisi hiyo la kuelimisha jamii namna ya kupambana na rushwa, katika uwanja wa mkesha wa mbio za mwenge wa Uhuru kata ya Maguu wilayani humo.