Monday, July 7, 2014

WANANCHI MKOANI RUVUMA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Rachel Stephen Kassanda akihutubia wananchi mbele ya Jengo la makaazi ya idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma, mara baada ya kulizindua katika kata ya  Mahenge Manispaa ya Songea. Amesema wapo wananchi wa mkoa wa  Ruvuma wanaoshirikiana na Wahamiaji haramu kuwasafirisha na kuwahifadhi katika maeneo maalumu  amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa idara hiyo ili kutokomeza vitendo hivyo.

Kiongozi mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Stephen Kassanda amesema wahamiaji walio wengi hutoka Eretria, Somalia hupitia mipaka ya mkoa wa Ruvuma.
Pichani anayehutubia ni kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014, anayefuatia katikati ni Afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza na wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti.

 Watumishi wa idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenge wa Uhuru katika jengo la makaazi la Afisa uhamiaji mjini Songea, lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Stephen Kassanda. Pichani aliye katikati ya viongozi wa mbio za Mwenge ni afisa uhamiaji wa mkoa huo Kokwi Lwebandiza.
Watumishi wa idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za Mwenge mara baada ya kuzindua jengo lao.
Mwenge wa Uhuru 2014 ukiwa na viongozi wa msafara wa mbio za Mwenge mkoani Ruvuma katika eneo la mradi wa jengo la makaazi ya uhamiaji, Mahenge Manispaa ya Songea. Wenye sare za kitenge ni kikundi cha kwaya kutoka wilaya ya Namtumbo.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa aliyeshika taarifa akiwa katika msafara wa mbio za Mwenge Manispaa ya Songea kushiriki katika uzinduzi wa miradi iliyokamilika katika halmashauri yake.
 Katika utunzaji wa mazingira mkoa wa Ruvuma, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Rachel Kassanda aliweza kupanda mti wa mkungu akiashiria kushiriki katika utunzaji wa mazingira.
 
 Afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akipokea Mwenge wa Uhuru ikiwa ni ishara ya uzalendo nchini Tanzania.
Baadhji ya maafisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda. kushoto ni Shaban, mmoja kati ya watumishi wa idara ya uhamiaji mkoani Ruvuma.

Hili ni jengo la uhamiaji mkoa wa Ruvuma lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, kitaifa lililogharimu kiasi cha shilingi 434,100,170. Lililopo Mahenge Manispaa ya Songea.


Pichani wa pili kutoka kulia afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza, akiwa na watumishi wa idara hiyo muda mfupi kabla ya msafara wa mbio za Mwenge wa Uhuru, kuwasili katika eneo la jengo la uhamiaji tayari kwa kuzindua.

Mhasibu idara ya uhamiaji mkoani Ruvuma, aliyeshika Mwenge katika eneo la jengo la makaazi ya uhamiaji mjini Songea. (Picha zote na Mwandishi wetu)

No comments: