Wednesday, March 27, 2013

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ROSE MAHENGE KUTUMBUIZA WANAMBINGA SIKU YA SHEREHE ZA PASAKA


Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.


MWIMBAJI wa muziki wa Injili kutoka wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, Rose Mahenge anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu mpya iitwayo Waweza zeeka mapema, siku ya sikukuu ya Pasaka Machi 31 mwaka huu kwenye ukumbi wa Uvikambi uliopo Mbinga mjini.

Akizungumza na Mtandao huu Mahenge anasema uzinduzi huo utashirikisha wasanii maarufu nchini, Senga na Pembe kutoka Jijini Dar es salaam ambao nao watakuwa wakitumbuiza na kutoa burudani za aina mbalimbali siku hiyo.


Mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu alisema albamu hiyo imebeba nyimbo kumi ambazo ni  Waweza zeeka mapema, Mbinguni tutaimba, Maajabu ya wanadamu, Leleno tuhine, Nasubiri zamu yangu, Mungu nikupe nini, Uumbaji wa Mungu, Makabila yote, Rimix(Mbinguni tutaimba) na Mwanaume ni Yesu.

Kwa mujibu wa msanii huyo alifafanua kuwa nyimbo hizo zimebeba maudhui yanayolenga na kumtaka binadamu kumcha Mungu na kuacha starehe na anasa mbalimbali ambazo zimekuwa zikisababisha ongezeko la dhambi duniani.

"Lengo hasa katika nyimbo hizi nataka pia watu tubadilike tuache dhambi na kutoa michango mikubwa kwenye sherehe kuliko kanisani", alisema.

Hiki ni kibao cha pili cha Injili kwa msanii huyo kukitoa ambapo awali alikuwa akitamba na kibao Mbinguni ndiko nyumbani kwetu, na kwamba alieleza kuwa katika uzinduzi huo, mgeni rasmi atakuwa Meneja wa benki ya CRDB tawi la Mbinga, Efrosina Mwanja.



No comments: