Friday, March 28, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE KUFUNGUA STENDI YA KISASA MBINGA


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma(katikati) Said Mwambungu akizungumza na viongozi waliokuwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Mbinga, wakati wakiwa katika eneo la stendi mpya ya abiria ambayo imejengwa mjini hapa.(Picha na Kassian Nyandindi)











Na Kassian Nyandindi,

Mbinga.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete anatarajia kufanya ufunguzi wa kituo kikuu cha stendi mpya ya magari ya abiria ambacho kimejengwa wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.

Ufunguzi huo utafanyika mwezi Mei mwaka huu wakati atakapokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alieleza hilo wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa wilaya ya Mbinga, katika ziara yake ya kikazi iliyofanyika hivi karibuni wilayani humo.

Mwambungu aliupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa ujenzi wa stendi hiyo iliyopo mjini humo, ambayo ni kitega uchumi kizuri cha kuiingizia mapato halmashauri ya wilaya hiyo.


Katika eneo hilo la stendi kumejengwa majengo makubwa mawili ya gorofa ambayo yamegharimu kiasi cha fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni 1.2 na sasa ujenzi wake umekamilika.

Pamoja na mambo mengine Mkuu huyo wa mkoa alifafanua kuwa kazi hiyo iliyofanywa na uongozi wa wilaya ya Mbinga, ni mfano mzuri wa kuigwa kwa viongozi wengine wa mkoa huo katika ubunifu wa miradi mbalimbali ya kuingiza mapato katika halmashauri zao.



No comments: