Rais Jakaya Kikwete. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
MALALAMIKO yaliyotolewa juu ya shilingi bilioni 2 ambazo baadhi ya
vyama vya ushirika (AMCOS) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, vilikopeshwa na
shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) na kuleta gumzo kuwa Mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri hiyo Hussein Ngaga, hakuzipeleka kwenye vyama hivyo badala yake
alidaiwa kuziingiza kwenye akaunti ya halmashauri ya wilaya hiyo tumebaini
kwamba, fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti husika za vyama hivyo huku akitoa
masharti kwa uongozi wa AMCOS hizo kuwa, hawana ruhusa ya kuzifanyia
matumizi ya kukopeshana mpaka idhini itoke kwake.
Aidha mkurugenzi huyo analalamikiwa kuwa viongozi hao wa vyama vya ushirika, alikuwa akiwapangia matumizi ya fedha hizo baada ya yeye
kujiridhisha kwanza wameandaa mpango kazi wa mahesabu husika na kiasi cha
kahawa walichonacho ambayo itaingizwa kiwandani, ndipo alikuwa akiwaruhusu kwenda kutoa fedha benki huku akihakikisha hundi
walizoandika zina kiwango halisi anachokifahamu.
Na wakati mwingine analalamikiwa kuwa, alikuwa hawapatii fedha kwa kiwango walichoomba katika mahesabu hayo ambayo walikuwa wakimpelekea ofisini kwake kwa ajili ya kuyakagua na kujiridhisha, badala yake alikuwa anapunguza kwa kiwango anachokitaka yeye.
Na wakati mwingine analalamikiwa kuwa, alikuwa hawapatii fedha kwa kiwango walichoomba katika mahesabu hayo ambayo walikuwa wakimpelekea ofisini kwake kwa ajili ya kuyakagua na kujiridhisha, badala yake alikuwa anapunguza kwa kiwango anachokitaka yeye.
Tumebaini pia baada ya mauzo ya kahawa kufanyika mnadani Moshi, hivi sasa mkurugenzi Ngaga amekuwa akikwepa kutoa Fomu ya
mauzo ya kahawa kwa dola (Account Sale) kwa wanaushirika hao, licha ya wao kumfuata mara kwa mara
wakimtaka awapatie.
Katika fomu hiyo huonyesha kahawa ambazo zimeuzwa kwa dola na ubadilishaji wa fedha za mauzo ya kahawa kutoka kiwango cha dola kuwa shilingi, hivyo inadaiwa huenda zimeuzwa kwa bei ya juu huku wanaAMCOS hao
wakimlalamikia kuwalipa bei ndogo, ndio maana hataki kutoa fomu hizo na kuweka mchakato
huo wa mauzo kuwa bayana ili wakulima waweze kufahamu juu ya mauzo ya kahawa yao
ulivyofanyika.
Hali hiyo imeelezwa na wakulima hao kuwa huenda anaficha ukweli
halisi usiweze kujulikana juu ya mwenendo mzima wa mauzo ya kahawa yao
ulivyofanyika huko mnadani kwa kila mkulima (vikundi).