Monday, January 6, 2014

TUNDURU WATAKIWA KUJENGA MSHIKAMANO NA UPENDO



Aliyesimama Diwani wa kata ya Majengo Athuman Nkinde akisisitiza jambo kabla ya kugawa vifaa vya kutengeneza batiki na sabuni za maji na vipande, kwa vikundi vya Majengo A na B wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma. Ambao wameketi ni viongozi wengine wa kata hiyo.  


Na Steven Augustino,
Tunduru.

WANACHAMA na wakereketwa wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Majengo wilayani Tunduru Ruvuma, wamehimizwa kudumisha muungano na upendo miongoni mwao na kuhakikisha wanapata ushindi wa  chama chao katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mariwani Athumani Nkinde wa Kata hiyo na  Diwani waviti maalumu wa tarafa ya Mlingoti Bi. Atingala Mohamed walisema hayo kwa nyakati tofauti  wakati wa  uzinduzi wa mradi wa maji safi ya bomba ugawaji wa vifaa vya kutengenezea Batiki, mafuta ya kupaka, sabuni za maji, na vipande katika kata hiyo.

Madiwani hao walisema kuwa endapo wanaCCM hawatashikamana katika ujenzi na uimarishaji wa chama chao ipo hatari ya mamluki kuingia miongoni mwao, na kuwavuruga kwa lengo la kuvipatia ushindi vyama pinzani.
 
Akifafanua taarifa ya ujenzi wa mtandao wa bomba la maji hayo na vifaa hivyo Diwani Athuman Nkinde, alisema kuwa hadi kukamilika kwake miradi hiyo imegharimu shilingi 400,000 na akatumia nafasi hiyo kuwaomba waitumie na kuitunza.


Mwenyekiti wa CCM wa kata ya Majengo Giramu Said naye alimpongeza diwani huyo kwa kujitoa wakati wote kuwawatumikia wananchi wake, na kuongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwapa moyo wananchi hao na kuendelea kuwa na imani naye.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita diwani huyo ametekeleza ahadi za kuanzisha miradi ya kuuza Kuni na mkaa unaosimamiwa na viongozi wa kata hiyo, mradi wa kilimo cha mpunga unaosimamiwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Kata hiyo.

 

No comments: