Na Mwandishi
wetu,
Tunduru.
WANACHAMA wapya 200 wamejitokeza wilayani Tunduru, mkoa wa
Ruvuma na kujiunga na Jumuiya ya Umoja Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi
(UWT) wilayani humo.
Fatuma Mandingo ambaye ni Katibu wa Jumuiya hiyo wilayani humo,
alisema huo ni mwanzo mzuri wa kuimarisha umoja wao hasa katika kuelekea kipindi
hiki cha uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Mandingo alisema kuwa UWT itagawa kadi kwa wanachama wapya wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru, ili kuendelea kuimarisha na kujihakikishia
ushindi katika uchaguzi huo ujao ambao wanachama wa CCM watamchagua Rais,
Mbunge na Diwani.
Katibu huyo alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini hapa, kwenye viwanja vya baraza la Idd ambao ulihudhuriwa na
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Ruvuma, Kuruthum Mhagama ambaye ndiye alihusika
katika kugawa kadi hizo kwa wanachama wake.
Alisema kuwa wanachama hao wamepatikana kupitia hamasa
iliyofanywa kupitia vikao vyao mbalimbali, na kwamba zoezi hilo ni endelevu.
“Tatizo kubwa tunalokabiliana nalo hapa ni upungufu wa kadi,
hivyo tunawaomba viongozi wetu wa UWT mkoa wafanye utaratibu wa kutuletea kadi
ili wanachama wengi waliopo ndani ya wilaya hii, waweze kuwa na kadi”, alisema
Mandingo.
No comments:
Post a Comment