Na Steven Augustino,
Tunduru.
WANAWAKE mkoani Ruvuma,
wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi mkoani
humo ili kuweza kufikia malengo ya hamsini kwa hamsini, katika kuongoza jamii.
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake ya Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) mkoani humo imewataka wanawake kufanya hivyo, kwa kuunganisha
nguvu pamoja na kuacha tabia ya kubezana au kupakana matope kwamba mtu fulani
hatoshi.
Hayo yalisemwa na
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani Ruvuma, Kuruthum Mhagama katika mkutano wa
hadhara, uliofanyika kwenye viwanja vya baraza la Idd wilayani Tunduru.
Alisema kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao, kitaibuka na ushindi wa kishindo
hivyo wanachama wa UWT wametakiwa kuendelea kukisemea vizuri chama hicho, hasa
kwa yale yaliyotekelezwa kupitia ilani yake.
Kadhalika Waasisi wa CCM
wilayani humo, Husna Makanjila na Futuma Kalongo walitahadharisha kuwa wajumbe
hao wanatakiwa kufanya kazi zao, kwa kuzingatia weledi na kuacha kukigawa
chama.
Walisema hivi sasa
kumekuwa na utitiri wa vyama vya siasa hapa nchini, ambapo muda mwingi vimekuwa
vikikiandama chama tawala kwa kutoa kauli mbaya na matusi, kwamba chama hicho
ambacho kimetawala watanzania miaka 50 hakijafanya chochote, jambo ambalo sio
kweli.
Waasisi hao walieleza
kuwa wanawake ambayo ndiyo nguzo kuu ya familia katika taifa hili, endapo
wataunganisha nguvu zao katika ushawishi kwa chama cha mapinduzi kutakuwa na
uhakika kuwa chama hicho kitaibuka na ushindi mnono kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Awali akifungua mkutano
huo Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tunduru, Mariam Mchongea aliwaeleza wapenzi na
wakereketwa wa CCM kuwa wanawake kupitia Jumuiya hiyo wamejipanga na
kuhakikisha kwamba, hapatakuwa na mpasuko wa aina yoyote ile ambao utasababisha
chama tawala kumeguka katika makundi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment