Na Steven
Augustino,
Tunduru.
MWANAFUNZI anayesoma darasa la saba shule ya msingi Msamaria,
iliyopo kijiji cha Mtangashari wilayanai Tunduru mkoa wa Ruvuma, Ramadhan Swedi
(14) amelazwa katika Hospitali ya wilaya hiyo, baada ya kuumwa na nyoka.
Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa, mwanafunzi huyo alikumbwa
na mkasa huo wakati akiwa anacheza mpira na wenzake katika maeneo ya shule
hiyo.
Mzazi wa
mwanafunzi huyo, Usale Swedi alisema baada ya tukio hilo kutokea walimu
walimpatia huduma ya kwanza ya kumfunga kamba na kumnywesha mafuta ya taa, na
baadaye kumpeleka nyumbani kwake.
Alisema, baada ya tukio hilo wanafamilia walilazimika kubeba
jukumu la kumpeleka hospitali, kwa matibabu zaidi ili kuokoa maisha
yake.
Swedi aliwapongeza waganga na wahudumu wa hospitali hiyo, kwa
jitihada walizozifanya utoaji wa huduma kwa mtoto huyo, ingawa bado wamelazwa
kwa ajili ya matibabu lakini hali yake inaendelea kuimarika.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Tunduru, Dkt. Mmari
Zabron alikiri kumpokea majeruhi huyo, Marchi 15 waka huu.
Alisema hivi sasa hali yake inaendelea vizuri na maofisa
tabibu, wanaendelea kumpatia matibabu ili kuokoa maisha yake.
No comments:
Post a Comment