Afisa afya wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Dokta Vitalis Mkomela hivi karibuni akikabidhiwa sehemu ya lita 1,000 za Viuawadudu toka kwa Waziri wa afya Dokta Ummy Mwalimu. |
ubwa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria.
Kufuatia hali hiyo tayari Manispaa hiyo
imepokea dawa hiyo na hivi sasa yanafanyika maandalizi ya kuanza kupulizia
makazi ya wananchi ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
Afisa afya na mazingira wa Manispaa
ya Songea Dokta Vitalis Mkomela alisema kuwa wamepokea lita 1,000 za dawa hiyo,
ambazo zimenunuliwa na Rais Dokta John Magufuli ambapo kiasi hicho cha dawa
kinatosha kupulizia katika kipindi hiki cha kiangazi katika mitaa 95 ya Manispaa
hiyo.
Dokta Mkomela alisema kuwa kabla ya
kuanza kazi ya kupulizia yanaandaliwa mafunzo na miongozo kwa wafanyakazi wa
kujitolea 95, wenyeviti wa mitaa 95 na maafisa afya ambao watapewa elimu ili
waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
“Idara itanunua pampu 98 zitakazotumika
katika zoezi hili, pia unahitajika usafiri ili wafanyakazi waweze kuanza kazi
mapema kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tano asubuhi”, alisema.
Vilevile alieleza kuwa mazalia ya mbu
yakipungua, mbu wa malaria pia watapungua na hatimaye ugonjwa huo utaweza
kufikia hatua ya kutokomezwa katika Manispaa hiyo.
Ili kuhakikisha zoezi hilo linatoa
matokeo makubwa Dokta Mkomela alisisitiza kuwa kila dimbwi la maji lenye
mazalia ya mbu litapuliziwa mara nne kwa mwezi sawa na kupulizia mfululizo kila
baada ya siku saba na kwamba watapulizia pia mazalia ya mbu yaliyofunikwa na yale
yaliyokuwa wazi.
Aliongeza kuwa zoezi hilo litakuwa
endelevu ambapo katika kipindi cha masika Manispaa itanunua dawa za kupulizia
mazalia yote ambayo yatakuwepo katika kipindi hicho ili kuhakikisha kuwa
mazalia ya mbu yanatokomezwa kabisa.
Hata hivyo jumla ya watu 133 katika halmashauri
ya Manispaa ya Songea mkoani hapa wamefariki dunia mwaka 2015 baada ya kuugua
ugonjwa wa malaria huku Watanzania 60,000 nao wanakufa kila mwaka kutokana na
ugonjwa huo ambapo pia kila siku hapa nchini watu 291 wamekuwa wakipoteza
maisha kutokana na malaria.
No comments:
Post a Comment