Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba. |
Na Mwandishi wetu,
WAZIRI wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la
Polisi hapa nchini kuziachia Pikipiki zote ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu,
na zile zenye makosa madogo pia waziachie wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zinafikia
hatua ya kuwa vyuma chakavu.
Mwigulu alisema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa
kivita, madawa ya kulevya na wale wanaotelekeza wabaki nazo wafanye utaratibu
wa kuwapeleka Mahakamani au kuziteketeza, na zile zenye makosa madogo watatue
haraka na kuwarudishia wenye zao huku wakiwapatia elimu wamekosea wapi.
“Wapeni masomo wamekosea wapi waelekezeni na waliowabishi warekebisheni
lakini tusirundike tukatengeneza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi
wake tunao, tutumie huu mkono kutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka
yetu”, alisema Mwigulu.
Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu
sheria ya usalama barabarani, ili kuweza kupunguza ajali za Pikipiki na
mrundikano wa Pikipiki katika vituo vya Polisi nchini kwani kila anapopita
vituo vya Polisi hukuta Pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogo madogo
ambayo yanaweza kutatuliwa.
No comments:
Post a Comment