Dokta John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
Na Mwandishi wetu,
DOKTA John Pombe Magufuli, ambaye ni Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa kauli yake akizungumzia juu ya kifo
cha mwanafunzi aliyepigwa risasi na Polisi, Februari 16 mwaka huu.
Katika ukurasa wake wa twitter, Rais
Magufuli ameandika ujumbe kuhusu kusikitishwa kwake na kifo cha Akwilina
Akwiline na kuagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatu waliohusika kufanya hivyo.
“Nimesikitishwa sana na kifo cha
mwanafunzi Akwilina Akwiline wa Chuo cha Usafirishaji (NIT),
“Natoa pole kwa familia, ndugu, wanafunzi
wa NIT na wote walioguswa na msiba huu,
“Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya
uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili”,
ameandika Rais Magufuli.
Kwa ujumla Akwilina alikuwa
mwanafunzi wa Chuo hicho jijini Dar es salaam, ambapo aliuawa kwa kupigwa risasi
na Polisi wakati wa vurugu za siasa zilizotokea siku ya Ijumaa, akiwa kwenye
daladala.
Kuhusu Mazishi
Serikali imetangaza kugharamia
mazishi ya mwanafunzi huyo aliyeuawa kwa kupigwa risasi, wakati wa maandamano
ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakishinikiza
Mkurugenzi wa Uchaguzi Kinondoni kutoa viapo kwa mawakala wa chama hicho.
Juu ya kugharimia mazishi hayo kauli hiyo
imesemwa leo Februari 18 mwaka huu na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es
salaam.
“Serikali imepata pigo kwani
inawekeza fedha nyingi kusomesha wanafunzi na marehemu Akwilina alikuwa ni
miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, tutagharamia shughuli zote za
mazishi ya marehemu hadi atakapopumzishwa katika makao yake ya milele”, alisema
Profesa Ndalichako huku akitoa onyo kwa Watanzania kuhusu kutofanya maandamano.
“Nawasihi Watanzania kujiepusha na
maandamano na vitendo vyote ambavyo vinaweza kusababisha uvujifu wa amani”,
alisema.
No comments:
Post a Comment