SERIKALI ya Tanzania imesema kwamba inajiondoa katika mpango wa
Umoja wa mataifa wa kusaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa
yanayowahifadhi.
Tanzania limekuwa eneo salama kwa wakimbizi wengi na sasa
inahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 wa nchi ya Burundi ambao walitoroka
mzozo.
Rais Dokta John Pombe Magufuli amesema kwamba taifa lake
linajiondoa kutokana na tatizo la usalama pamoja na lile la kifedha.
.Uganda yakana kutaka kuwafurusha wakimbizi wa Burundi
.Tanzania inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi
.Nkurunziza afika Tanzania ziara yake ya kwanza nje tangu
2015
Mwaka uliopita taifa hilo lilisimamisha kwa muda usajili wa
wakimbizi wapya na kuwataka wakimbizi wa Burundi kurudi nyumbani, hatua ambayo
ilishtumiwa na makundi ya kupigania haki za kibinadamu.
Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa kinasema kuwa kinatuma
ujumbe wa ngazi za juu kwa mazungumzo na Serikali ya Tanzania.
Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka
Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbizi la Umoja
wa Mataifa UNHCR.
Ripoti hiyo inasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi laki 2 na
elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.
Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR
inasema asilimia 60 ni watoto.
Na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017,
wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania.
UNHCR inasema huu ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa
bahati mbaya, nchi hii haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na
wengine wanaotafuta hifadhi.
Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu ambayo inatajwa kuwa ni
moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000 idadi
ambayo inapaswa kupunguzwa na kuwagawa wakimbizi katika kambi nyingine.
Lakini hili limeshindikana, ripoti ya UNHCR inasema, na ni
kwasababu ya kukosekana kwa ardhi ya kufungua kambi mpya.
Source:BBC
No comments:
Post a Comment