Na Mwandishi wetu,
WATANZANIA wawili wamekamatwa nchini
China, January 19 mwaka huu wakiwa wamemeza dawa za kulevya tumboni kwenye
uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupamba na dawa za kulevya nchini,
Rogers Siang’a aliwataja watuhumiwa hao ni Baraka S. Malali na Mkewe Ashura H.
Mussa ambapo wamekamatwa wakiwa na mtoto wao mdogo mwenye umri wa miaka 2 na
miezi 9.
Kamishna Siang’a alisema kuwa baada
ya kukamatwa walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda, ndipo Baraka alitoa
Pipi 47 kwa njia ya haja kubwa huku Ashura akitoa Pipi 82.
Siang’a alieleza kuwa Serikali ya
China iliwasiliana na Serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo,
ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo hapa nchini.
Mamlaka ya kupambana na dawa za
Kulevya ikishirikiana na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na
ndugu wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwa ndugu zake ili aweze
kuendelea kupata matunzo.
No comments:
Post a Comment