Na Mwandishi wetu,
VIONGOZI Waandamizi wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) wameitwa na Jeshi la Polisi wakitakiwa kwenda kuripoti
leo jioni Februari 19 mwaka huu.
John Mrema ambaye ni kiongozi wa
Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje kwa chama hicho alithibitisha hilo kwamba
wameitwa kwa barua hiyo ambayo wameipokea makao makuu ya chama majira ya saa
kumi jioni.
Ambapo barua hiyo inawataka kwenda
kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam katika Ofisi yake.
Mrema alifafanua kuwa viongozi hao
waliotakiwa kwenda kuripoti huko wameshindwa kufika kituo cha Polisi, kwa kile
alichodai kucheleweshwa kwa barua hiyo kwani imewafikia saa kumi na dakika 51
na ikisema viongozi hao wafike saa kumi na moja jambo ambalo limeshindikana
kutokana na ukweli kwamba viongozi hao wanaishi katika maeneo mbalimbali hivyo
isingewezekana kuwapata wote ndani ya dakika tisa.
“Cha ajabu walikuwa wanawataka
viongozi hawa saa kumi na moja kamili jioni hivyo kulikuwa na dakika tisa tu
wakati viongozi wanaowataka ni wengi na wamesambaa maeneo mbalimbali,
“Hivyo wanasheria wetu wanashughulika
kuwajulisha Jeshi la Polisi juu ya hilo kwa sababu kama Mbunge John Heche ni
Mbunge wa Tarime, Esther Matiko na Mbunge wa Tarime hawa watu wamesambaa sasa
huwezi kuleta barua Makao makuu halafu utegemee kuwapata saa kumi na moja jioni,
“Yaani dakika tisa wawe wamewasili Polisi,
hivyo Mawakili wetu watawajulisha Polisi, na wale watakaopatikana na kuwajuza
wataripoti saa ngapi”, alisema Mrema.
No comments:
Post a Comment