Na Mwandishi wetu,
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Seleman Jaffo, amegoma kuzindua mradi
wa maji katika kijiji cha Itiso Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kutokana na
baadhi ya wananchi kuharibu kwa makusudi miundombinu hiyo.
Seleman Jaffo. |
Akizungumza na wananchi wa kijiji
hicho, Waziri huyo alisema kuwa awali mkandarasi aliyekuwa akijenga mradi huo alikuwa
akisuasua na kwamba Halmashauri ya Chamwino iliamua kumbadilisha Mhandisi wa
maji, ili kuweza kukamilika kwa haraka ujenzi wake na wa kiwango chenye bora.
Imeelezwa kuwa wananchi wa kijiji cha
Itiso wamekuwa hawana ushirikiano mzuri na viongozi wao na wale waliokuwa
wakijenga mradi jambo ambalo limekuwa likisababisha uwepo wa uharibifu wa miundombinu
hiyo ya maji.
Kufuatia hali hiyo alimuagiza Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino, Athuman Masasi kusimamia jambo hilo
kikamilifu na wale waliohusika kuharibu miundombinu hiyo washughulikiwe haraka.
Pamoja na mambo mengine, naye Mkurugenzi
huyo wa Halmashauri hiyo alisema kuwa licha ya Serikali kugharimia kiasi
kikubwa cha fedha kujenga mradi huo, lakini wananchi hao ndiyo wamekuwa mstari
wa mbele kuharibu miundombinu hiyo ya maji.
No comments:
Post a Comment