Na Kassian Nyandindi,
Songea.
MKAZI mmoja wa kijiji cha Luhimba kata ya Mtyangimbole wilaya
ya Songea mkoani Ruvuma, Allan Kihwili (48) ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi
mkoani humo kwa tuhuma ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita, ambaye
anasoma shule ya msingi Ngembambili na kumsababishia maumivu makali katika
sehemu zake za siri.
Zubery Mwombeji. |
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa mkoa
huo, Zubery Mwombeji alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 24 mwaka huu
majira ya saa 11 jioni katika kijiji hicho wilayani hapa.
Mwombeji alifafanua kuwa inadaiwa siku ya tukio hilo mwanafunzi
huyo ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa anapita jirani na nyumba ya mtuhumiwa
huyo ghafla alimkamata na kumwingiza kwenye nyumba anayoishi kisha kumfanyia unyama
huo.
Alibainisha kuwa mbinu aliyoitumia mtuhumiwa Kihwili ni
kwamba alikuwa akimvizia mtoto huyo wakati anapita kwenye eneo la nyumba yake,
akimtaka amuulize maswala ya shuleni anakosoma ndipo alipofanikiwa kumkamata na
kumwingiza ndani ya nyumba yake hatimaye kumfanyia ukatili huo.
Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi hapa mkoani Ruvuma alisema
kwamba uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo kinaonesha
kumekuwa na imani za ushirikina ambazo zilimfanya mtuhumiwa amfanyie kitendo
cha kinyama msichana huyo, ambapo Jeshi hilo linaendelea kufanya upelelezi wa
kina kuhusiana na tukio hilo ili mtuhumiwa aweze kufikishwa Mahakamani kujibu
shitaka linalomkabili mbele yake.
No comments:
Post a Comment