Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani
Ruvuma limewafukuza kazi baadhi ya watumishi wake, kutokana na makosa
mbalimbali yakiwemo ya utoro kazini na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya
shilingi milioni 46,680,000.
Nchimbi alisema kuwa waliofukuzwa kazi ni Mosta Ndunguru
ambaye ni Afisa tabibu na Bapara Mwang'ombe Mhudumu wa afya ambapo wote kwa
pamoja wamefukuzwa kwa makosa ya utoro kazini.
Aliwataja wengine waliofukuzwa kazi kwa kosa la kuisababishia
halmashauri hiyo ya Mbinga hasara ya shilingi milioni 46,680,000 kuwa ni
watumishi wawili ambao ni maofisa misitu wasaidizi, Kelvin Haulle na Ally
Almasi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Anyitike
Kasongo ambaye alikuwa ni Kaimu Mhandisi idara ya ujenzi, amevuliwa madaraka
hayo kutokana na kushindwa kusimamia kikamilifu miradi ya ujenzi wa nyumba za
walimu katika kata ya Kitura wilayani humo.
Vilevile aliwataja wengine ambao nao walikuwa wamesimamishwa
kazi kutokana na sababu mbalimbali na baraza hilo limewarejesha kazini kuwa ni
Ahsante Luambano aliyekuwa Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Said
Almasi ambaye ni Fundi sanifu idara ya ujenzi, Kebrina Tembo Afisa mtendaji wa
kata, Cosmas Mmasai, Mhasibu daraja la pili na Emmanuely Kapinga Afisa utumishi
ambaye amefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya uzembe kazini.
No comments:
Post a Comment