Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
IMEELEZWA kuwa hadi kufikia Disemba mwaka jana, mashamba
yenye ukubwa wa ekari 78,149.065 sawa na hekta 31,259.626 yameingizwa na
kupimwa katika mpango wa upimaji ardhi, ambapo halmashauri ya wilaya ya Mbinga katika
kipindi hicho imefanikiwa kupima ekari 70,491.165 na ekari 7,657.9 zimepimwa
kutoka halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa takwimu hizo na taarifa zilizomfikia mwandishi
wetu kutoka vyanzo mbalimbali vya habari vimethibitisha kuwa, halmashauri hizo
zinaendelea kutekeleza sheria za ardhi pamoja na kutimiza agizo la serikali la
kupima kila kipande cha ardhi na kukimilikisha kwa walengwa husika.
Aidha halmashauri zimekuwa zikiendelea kuhamasisha wamiliki
wa viwanja na mashamba kulipia kodi za ardhi pamoja na kuviendeleza viwanja
vyao kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kusambaza hati za madai ya kodi
kwa wadaiwa sugu na kwamba wale wanaoshindwa kulipa hufikishwa Mahakamani.
Vilevile kwa lengo la kuepuka migogoro ya ardhi katika
upangaji, upimaji na ugawaji wa viwanja baina ya wamiliki wa ardhi na serikali
wilaya ya Mbinga imekuwa ikitumia utaratibu wa upimaji shirikishi, bila kulipa
fidia ambapo mmiliki wa ardhi huchangia gharama ya upimaji kwa kutoa asilimia
40 ya viwanja vitakavyopatikana katika ardhi yake.
Utoaji wa asilimia hiyo ya viwanja huenda kwa halmashauri kwa
lengo la kufidia maeneo yote yatakayoangukia kwenye maeneo ya huduma za kijamii
kama vile barabara, maeneo ya wazi, ujenzi wa zahanati, masoko na shule huku
asilimia 60 ya viwanja itakayopatikana katika ardhi husika hubaki kwa mmiliki
wa ardhi.
Pia kwa mwaka wa fedha 2016/2017 nayo halmashauri ya mji wa
Mbinga, imeweza kufanikiwa kupima jumla ya viwanja 386 kwa kutumia utaratibu
huo wa upimaji shirikishi.
Halmashauri ya mji wa Mbinga inaendelea na jitihada za
kujiongezea mapato ya ndani kwa kupima viwanja vya matumizi mbalimbali ambapo
hadi kufikia Disemba mwaka jana, viwanja 55 vimepimwa katika eneo la uwanja wa
ndege lililopo mjini hapa na kazi hiyo bado inaendelea.
Kwa mujibu wa nakala ya taarifa ya maendeleo ya wananchi
ambayo nakala yake tunayo, inasisitiza kuwa mji huo unaendelea kufanya uthamini
wa majengo ili kuwezesha kutoza kodi ya majengo (Property Tax) kulingana na
thamani ya jengo husika.
Pamoja na mambo mengine kwa upande wa utatuzi wa migogoro mbalimbali ya ardhi wilaya ya Mbinga na halmashauri ya mji huo, imekuwa ikiendelea kupambana na utatuzi wa migogoro hiyo kwa kutenga siku moja ya Ijumaa ya kila mwisho wa mwezi na kuanzisha dawati la kupokea kero za wananchi zinazohusiana na masuala ya ardhi.
Pamoja na mambo mengine kwa upande wa utatuzi wa migogoro mbalimbali ya ardhi wilaya ya Mbinga na halmashauri ya mji huo, imekuwa ikiendelea kupambana na utatuzi wa migogoro hiyo kwa kutenga siku moja ya Ijumaa ya kila mwisho wa mwezi na kuanzisha dawati la kupokea kero za wananchi zinazohusiana na masuala ya ardhi.
No comments:
Post a Comment