Na Dustan Ndunguru,
Mbinga.
Mbinga.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma
Ambrose Nchimbi amewahakikishia wananchi wa kata ya Kitura wilayani humo kwamba
halmashauri hiyo itajenga daraja la mto Kitura ambalo limekuwa kero kubwa kwa
wananchi wa kata hiyo, sambamba na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto
zingine ambazo zimekuwa zikikwamisha shughuli za maendeleo ndani ya kata hiyo.
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri wilaya Mbinga, Gombo Samandito. |
Alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi hiyo ambayo
imekuwa ikitekelezwa kwa nyakati tofauti wilayani humo, sambamba na kubaini
changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo na
kwamba wananchi amewaasa kutoa ushirikiano wa karibu kwa kueleza ukweli hasa
pale wanapobaini mradi unatekelezwa chini ya kiwango.
Nchimbi alisema kuwa muda mrefu wananchi wa kata hiyo
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa barabara ya uhakika
hususani ile inayotoka Mbinga kwenda Litembo hadi Nkiri, ambayo ipo chini ya Wakala
wa barabara mkoa wa Ruvuma (TANROADS) ambayo hivi sasa imesahaulika kutokana na
kutofanyiwa matengenezo ya uhakika mara kwa mara na hivyo kuwa kero kubwa kwa
wananchi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitura, Areus Nguhi
aliwashukuru Wajumbe wa Kamati ya uongozi na mipango kwa uamuzi wake wa
kuitembelea kata hiyo na kuona changamoto mbalimbali zilizopo, ambazo wananchi
wamekuwa wakikabiliana nazo na kwamba yeye atahakikisha anatekeleza maagizo
yote muhimu ambayo yameelekezwa na Wajumbe hao ili kutatua kero ambazo zimekuwa
kwa muda mrefu zikiwakabili wananchi wa kata hiyo.
Nguhi alisema kuwa wananchi wake wamekuwa wakijitokeza kwa
wingi katika kuchangia nguvu zao kwenye shughuli za maendeleo hivyo aliiomba
halmashauri kuhakikisha inapeleka vifaa vya viwandani kwa wakati, ili
kukamilisha ujenzi wa majengo ambayo nguvu hizo zimetumika na hivyo kuyanusuru
yasiweze kubomoka hasa katika kipindi hiki cha masika ambacho mvua nyingi
hunyesha.
No comments:
Post a Comment