Wageni mbalimbali wakiwa katika eneo la viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Vita vya Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma. |
Songea.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Profesa Jumanne Maghembe ameshangazwa na utajiri wa vivutio vya utalii
vilivyopo katika mkoa wa Ruvuma, wakiwemo aina ya samaki wa mapambo zaidi ya
400 katika ziwa Nyasa mkoani humo na viumbe wengine adimu waliopo katika ziwa
hilo.
Kwa ujumla viumbe hao licha ya kuwa
ni adimu pia wamekuwa hawapatikani sehemu yoyote ile hapa duniani.
Profesa Maghembe alishangazwa na
hayo wakati alipokuwa akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 110 ya
Vita vya Majimaji, zilizofanyika kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya
Majimaji Songea mkoani hapa.
Alisisitiza kuwa ni fursa pekee
sasa, kuendelea kutangaza vivutio hivyo ili viweze kuleta tija kwa Taifa hili
kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho wakiwemo Wananyasa na mkoa wa Ruvuma
kwa ujumla.
Kwa ujumla ziwa Nyasa lipo katika
wilaya ya Nyasa mkoani humo ambapo licha ya kuwepo kwa samaki hao pia kumekuwa
na vivutio vingi vya utalii kama vile visiwa vya kuvutia vilivyopo kwenye ziwa
hilo, milima na mawe mazuri ya kuvutia ambayo yana historia nzuri za kale kwa
watu wanaokwenda kutembelea huko kujifunza mambo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment