Profesa Ibrahimu Juma. |
Na Ferdinand Shayo,
Arusha.
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma ameonesha kutoridhishwa
kwake na mfumo wa utoaji wa taarifa mbalimabli za Kimahakama ikiwa ni pamoja na
matamshi ya lugha, urasimu unaofanywa na baadhi ya Watumishi wa Mahakama katika
utoaji wa nakala za hukumu.
Profesa Juma ametoa kauli hiyo leo jijini Arusha katika
ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji na wataalamu wa Mahakama, kwa lengo la
kutathimini utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano na utekelezaji wa
mradi wa maboresho wa utoaji wa huduma za Mahakama hapa nchini.
Katika kikao hicho Jaji Mkuu, alitolea mfano andiko la benki
ya dunia linalozungumzia ukosefu wa taarifa kwa umma kuhusu mashauri na kasi
ndogo ya kuchapishwa kwa nakala za hukumu, huku nakala hizo zikichapishwa kwa
lugha ya kiingereza na wakati mwingine kisheria zaidi.
Vilevile katika kuitathimini taarifa ya benki ya dunia kuhusu
utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania, alisema meagiza kila Mahakama kuwa na
miongozo kwa watumiaji wa chombo hicho ili kuwasaidia wakati wa utafutaji wa
huduma mbalimbali za kimahakama.
Mpango unaojadiliwa na watendaji hao wa ngazi mbalimbali za
kimahakama ni ule wa miaka mitano kuanzia mwaka 2015/2016 hadi 2019/2020
unaofadhiliwa na benki ya dunia ukilenga maboresho ya utoaji wa huduma za
kimahakama hapa nchini.
No comments:
Post a Comment