Na Albano Midelo,
Songea.
KATIKA Manispaa ya Songea Mkoani
Ruvuma, Mradi wa machinjio ya kisasa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa
gharama ya shilingi zaidi ya bilioni tatu, unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi
Juni 30 mwaka huu.
Mradi huo unajengwa katika kata ya
Tanga iliyopo kwenye Manispaa hiyo hadi sasa umefikia karibu ya asilimia 80 ujenzi
wake, ambapo Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo ni Kampuni ya Giraffe ambayo imeahidi
kukamilisha kazi hiyo kabla ya tarehe ya mwisho wa mkataba ambao umeanzia Julai
2017 na kukamilika Julai 2018 mwaka huu.
“Imebakia mistari michache
kukamilisha kuzungusha jengo lote kisha tunaanza kazi ya kuezeka machinjio,
hadi mwishoni mwa mwezi Mei tunatarajia kazi itakuwa katika hatua za mwisho”,
alisema.
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Baraza
la Madiwani la Manispaa ya Songea, tayari imekagua mradi huo na kujiridhisha na
kasi ya ujenzi huku wakisema kuwa wanaamini atamaliza kazi hiyo kwa wakati
uliopangwa kwa mujibu wa mkataba husika.
Manispaa hiyo imelalamikia pia hivi karibuni
Televisheni moja binafsi imetangaza habari ambazo sio sahihi kwamba, ujenzi wa
machinjio hiyo unasuasua na kwamba Mkandarasi yupo nyuma ya mkataba jambo
ambalo wamesema kuwa sio la kweli na ni upotoshaji katika jamii.
Rai imetolewa kuwa wanahabari
kuhakikisha kwamba kabla ya kutangaza au kuchapisha habari wanapaswa kufanya
utafiti ikiwemo kwenda hadi eneo husika ili kuweza kupata ukweli wa habari
husika na hatimaye kutoa taarifa sahihi.
No comments:
Post a Comment