Baadhi ya mitambo mbalimbali na magari yaliyopigwa mnada na Manispaa Songea Mkoani Ruvuma. |
Na Kassian Nyandindi,
Songea.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea Mkoani
Ruvuma, Machi 24 mwaka huu imeuza kwa njia ya mnada wa hadhara mitambo yake 16
ikiwemo magari, pikipiki na mitambo mingine chakavu na kufanikiwa kukusanya
zaidi ya Shilingi Milioni 87.75.
Mitambo hiyo ambayo imeuzwa katika
mnada huo ni Mitsubishi Bozer, Toyota land Cruiser station wagon mbili, Nissan
station wagon, Nissan station wagon tipper, Isuzu tipper mbili, Hyster Roller, pikipiki
sita aina ya Suzuki 125, pikipiki aina ya Honda 110 na Hysosung.
Fedha hizo taslimu ambazo
zimekusanywa katika mnada huo uliofanyika kwenye Karakana ya Manispaa ya Songea
na kusimamiwa na Kampuni ya YONO Auction Mart chini ya dalali mahiri, Zuberi
Lumbizi ni shilingi zaidi ya milioni 26.
Kiasi hicho cha fedha taslimu kilichopatikana
ni moja ya masharti ya mnada ambapo Mnunuzi alitakiwa kulipa amana ya fedha
taslimu sio chini ya asilimia 25 ya thamani ya gari, pikipiki au mtambo
atakaoununua na kukamilisha malipo yote katika muda wa siku 28 kuanzia tarehe ya
mnada.
No comments:
Post a Comment