Tuesday, October 30, 2012

CCM YAIBUKA KIDEDEA RUVUMA


                       








Bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)


Kassian Nyandindi,


Songea.
 

CHAMA cha mapinduzi(CCM) mkoani Ruvuma, kimeibuka kidedea baada ya kuvibwaga vyama vya upinzani CHADEMA na CUF katika uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani uliofanyika kata za Mpepai na Mletele.

Katika kata ya Mpepai iliyopo wilayani Mbinga, mgombea wa CCM Bw. Francis Nchimbi aliibuka mshindi baada ya kujizolea kura 1449, Bw. Romanus Mbena wa CHADEMA alipata kura 289 na Bw. Bosco Ndunguru wa CUF alipata kura 44.



Kata ya Mletele iliyopo Manispaa ya Songea, mgombea wa CCM Bw. Maurus Lungu alitangazwa mshindi baada ya kujipatia kura 950 huku mgombea wa CHADEMA Bw. Leokardo Mapunda akiambulia kura 295.


Mara baada ya matokeo kutangazwa wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo kata ya Mpepai wilayani Mbinga, waliendeleza vitendo vyao vya vurugu ambapo kikosi cha kutuliza ghasia kilidhibiti vurugu hizo na amani iliendelea kutawala.

Wafuasi hao wa CHADEMA walikuwa wakitoa maneno ya matusi kwa viongozi wa CCM, lakini wafuasi wa chama hicho walikuwa wakiendelea kusherehekea ushindi walioupata.


 



No comments: