Wednesday, October 31, 2012

MGOGORO WA ZIWA NYASA UMALIZWE KWA AMANI














Ziwa Nyasa ambalo lina mgogoro kati ya Wamalawi na Watanzania (Picha na Mwambije blog).  

MALAWI NA TANZANIA:

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiendelea kuwepo kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mzozo wa mpaka ambao umekuwa kwa miaka mingi lakini sasa umefika daraja la juu huku viongozi wa nchi hizo mbili wakiendelea kuumiza vichwa juu ya uhalisia wa mpaka huo.

Mzozo unahusu umiliki wa ziwa Malawi ambalo ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika na ambalo linapakana na nchi ya Malawi, Tanzania na Msumbiji.

Tangu miaka ya sitini Tanzania na Malawi nchi hizi zimekuwa zikizozana kuhusu umiliki wa ziwa hilo, lakini mgogoro huu kwa sasa umekuwa ukijenga hofu kwa wananchi kutokana na kudaiwa kuwepo kwa gesi na mafuta katika ziwa hilo.

Msumbiji mpaka sasa haijahusika kwa namna moja au nyingine katika kujihusisha na mzozo huu.


Nini hasa kinazozaniwa?
 
Fahari ya nchi na maswala ya kujiendeleza kiuchumi kwa Malawi na Tanzania kila mmoja akisimama kidete kusisitiza msimamo wake.

Kwa Tanzania ziwa hilo linajulikana kwa jina la Nyasa, wakati nchini Msumbiji linajulikana kwa Lago Niassa mmalawi analiita ziwa Malawi.

Malawi na Tanzania ni koloni za zamani za Uingereza wakati Msumbiji ilikuwa chini ya ukoloni wa Ureno. Uingereza iliichukua Tanzania kutoka kwa Wajerumani baada ya wao kushindwa katika vita vya kwanza vya dunia.
Kando na ripoti za kuwepo mafuta na gesi katika ziwa hilo, ziwa lenyewe ni kivutio kikubwa cha watalii.

Malawi inasema inashauriana na Msumbiji kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika siku za baadaye ili kuzuia mzozo wa kidiplomasia .
 
Je hii ni mara ya kwanza kwa mzozo huu wa ziwa Malawi kutokea?
 
Jibu ni Hapana.

Ukweli halisi:

Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania.

Makubaliano hayo yaliafikiwa na Muungano wa Afrika, na Tanzania ikaitikia ingawa shingo ilikuwa kwa upande. Mzozo mpya kati ya nchi hizo ukaripotiwa tena kati ya mwaka 1967 na 1968 na sasa ndio umenza kuibuka tena upya. (Posted by Mwambije blog)

 
 

No comments: