Thursday, September 18, 2014

DEREVA PIKIPIKI AKUTWA AMEFARIKI DUNIA BAADA KUCHOMWA KISU TUMBONI



Na Kassian Nyandindi,
Songea.

MTU mmoja ambaye ni dereva wa pikipiki amekutwa amefariki dunia baada kuchomwa kisu tumboni na kupigwa na kitu kizito kichwani kisha mwili wake kufungwa kamba mikononi na miguuni hatimaye kuunganishwa kwenye mti na watu wasiojulikana.

Tukio hilo lilitokea Septemba 16 mwaka huu majira ya mchana ambapo mwili wa marehemu huyo umetambuliwa kwa jina la Maulid Kuburi (21) mkazi wa kijiji cha Mpandangindo Songea vijijini mkoani Ruvuma.

Mwili wa marehemu huyo umekutwa na majeraha ambapo alichomwa kisu mara tatu tumboni kisha kufariki dunia.


Aidha uchunguzi wa awali unaonesha mnamo Septemba  13 mwaka huu, majira ya mchana marehemu akiwa kijijini kwake Mitawa, akiwa na pikipiki yake yenye namba za usajili T 850 CMT aina ya SANLG alikodiwa na watu wawili wasiojulikana ambao walishuka kwenye gari lililokuwa linatoka barabara ya Njombe kwenda Songea, tangu hapo hakuonekana tena mpaka umauti ulipomkuta.

Juhudi za kuwatafuta wahusika wa tukio hilo zinaendelea na jeshi la polisi mkoani humo, na kwamba linatoa rai kwa wananchi wote kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu na vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

No comments: