Wednesday, September 10, 2014

SERIKALI YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUUZA MAHINDI NJE YA NCHI



Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.

SERIKALI hapa nchini imeruhusu wafanyabiashara kuuza mahindi yao nje ya nchi popote pale, huku ikiwataka kuzingatia bei elekezi iliyowekwa ili kumfanya mkulima asiweze kupata hasara.

Sambamba na hilo mahindi ambayo yamehifadhiwa katika vituo husika vilivyopo mkoani humo, serikali itayanunua kwa kilo shilingi 500 na kwamba wakulima hawaruhusiwi kuingiza mahindi mengine katika vituo.


Mkurugenzi wa mipango na uendeshaji kutoka makao makuu ya mamlaka ya hifadhi ya chakula Tanzania (NFRA), Anna Ngoo alisema hayo wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma akikagua mahindi ambayo yamehifadhiwa katika vituo husika mkoani humo.

“Mahindi yaliyopo sasa katika vituo hivi vya kununulia yasiingizwe tena, serikali ipo tayari kuyanunua haya tu yaliyopo sasa”, alisisitiza.  

 Vilevile Ngoo aliwataka wakulima hapa nchini katika maeneo ambayo mahindi yanazalishwa kwa wingi, wajiunge katika vikundi ili serikali iweze kununua zao hilo kwa urahisi. 

“Wakulima hawa wakiwa pamoja na serikali ikatekeleza majukumu yake hizi kelele za kutaka tununue mahindi yote waliyozalisha hazitakuwepo tena, tuwaelimishe wajiunge pamoja”, alisema Ngoo.

No comments: