Na Steven Augustino,
Tunduru.
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma, limewataka viongozi wa serikali katika vijiji vya wilaya hiyo kutoa
hamasa kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi, kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa kieletroniki (BVR).
Mwenyekiti wa baraza hilo la Madiwani la wilaya hiyo, Faridu Khamis alitoa
rai hiyo alipokuwa akizungumza nao katika kikao walichoketi ukumbi
wa Klasta ya walimu, tarafa ya Mlingoti mjini humo.
“Uhamasishaji wa wananchi waweze kujitokeza na kujiandikisha ni
jambo la lazima ndugu zangu, jitahidini kuwahamasisha ili tuweze kufikia lengo
husika”, alisisitiza.
Akizungumzia juu ya maendeleo ya zoezi hilo, Faridu alisema
tayari kata kumi zilizopo kwenye tarafa ya Mlingoti limeonekana wananchi wake
kuwa na hamasa wakijitokeza kwa wingi na kusababisha hata baadhi yao, kukimbilia
vijiji jirani kwenye watu wachache ambao walijitokeza kujiandikisha.
Pia akitoa salamu za serikali kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya
Tunduru, Chande Nalicho ambapo katibu tawala wa wilaya hiyo, Ghaibu Lingo
alifafanua kwa kuwataka wananchi waondokane na dhana kwamba kutakuwa tena na
muda wa kuwaongezea kujiandikisha badala yake wanapaswa kulitekeleza hilo sasa, kwa
kujitokeza kwa wingi na sio vinginevyo.
Jumla ya vituo 214 ambavyo vimegawanywa katika kata za wilaya
hiyo, vimezingatia jiografia ya wilaya ambapo vituo 53 vinafanya kazi katika kata husika, kati
ya mashine za BVR kit 74 zilizopokelewa.
No comments:
Post a Comment