Na Steven Augustino,
Tunduru.
SERIKALI wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, imewahimiza wananchi wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili waweze kupata vitambulisho vya kitaifa.
SERIKALI wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, imewahimiza wananchi wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili waweze kupata vitambulisho vya kitaifa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Chande Nalicho
wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo ambalo lilifanyika kwenye ofisi za mkuu huyo
wa wilaya, zilizopo mjini hapa.
Nalicho alifafanua kuwa miongoni mwa faida za vitambulisho
hivyo, ni pamoja na kila Mtanzania kutambuliwa kadhalika kitakuwa na msaada
mkubwa kwa mtu binafsi hasa pale anaposafiri nje ya nchi.
Alisema kuwa wito huo ameutoa kwa wananchi wake wa wilaya
hiyo, kutokana na kuwa pembezoni mpakani mwa Tanzania na Msumbiji hivyo kuwepo
kwa vitambulisho hivyo kutasaidia hata mamlaka husika, kuwatofautisha wananchi
wake kutokana na muingiliano uliopo miongoni mwao.
“Kitambulisho hiki ni muhimu sana, hasa kwa upande wetu wa
Tanzania maana wenzetu nchi jirani ya Msumbiji tayari wao wamekwisha jiandikisha
na kupatiwa”, alisema.
Awali akitoa taarifa za uanzishwaji wa zoezi hilo, Ofisa wa
shirika la NIDA wilaya ya Tunduru Anafi Nachungu alisema kuwa shirika hilo
litafanya zoezi hilo la utambuzi na usajili wa watu wilayani humo, kuanzia kwa
watumishi wa serikali na baadaye kwa wananchi wa kawaida.
Zoezi hilo ambalo limeanza Aprili 24 mwaka huu, kwa kujaza
fomu na kuchukua alama za vidole vya Mkuu huyo wa wilaya, limepangwa
kutekelezwa kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusuambao unatarajiwa kuishia
mwanzoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.
Nachungu aliendelea kufafanua kuwa katika kipindi hicho, yeye
na wasaidizi wake Dainas Mossy na Salvatory Majengo wamejipanga na kuhakikisha
kuwa zoezi hili ambalo lilikwama kuanza mwezi Agosti 2014, linakamilika mapema
na kwa wakati.
No comments:
Post a Comment