Na Mwandishi wetu,
Tunduru.
TIMU ya Stendi FC Tunduru mjini mkoani Ruvuma, imetawazwa
kuwa bingwa ligi ya kuitangaza Hoteli mpya ya Peace and Love iliyopo mjini
hapa, baada ya kuwachapa magoli mawili kwa moja, mahasimu wao wa timu ya
Usalama FC ya mjini humo.
Mchezaji Shaban Chitepete, ndiye aliyefungua milango ya
wapinzani hao baada ya kuifungua timu yake kwa goli la kwanza ambalo lilitikisa
nyavu za wapinzani wao katika dakika, ya 21 huku la pili likigonga tena nyavu
hizo kwa dakika ya 23 ambalo lilifungwa na Exavia Chimgege, mchezo ambao
ulikuwa ukisakatwa katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi mjini Tunduru.
Upande wa usalama FC goli la kufuta machozi lilifungwa na
Fakihi Maliyatembo, katika dakika ya 39na kuwahadaa walinzi wa Stendi FC baada
ya kufyatua mkwaju mkali, ambao ulimwacha golikipa wa timu hiyo njia panda.
Akizungumzia juu ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha
mpira wa miguu (TDFA) wilaya ya Tunduru, Kitwana Mzee alisema ligi hiyo ambayo
ilianza Aprili 9 mwaka huu kwa kushirikisha timu 12 kutoka ndani ya wilaya
hiyo.
Kitwana aliendelea kufafanua kuwa, katika mashindano hayo
timu hizo ziligawanywa katika makundi mawili A na B huku wakicheza kwa mtindo
wa mtoano ambapo katika hatua ya awali, timu sita ndizo zilizofanikiwa kuingia
katika awamu ya pili na kupangwa kucheza katika mpango wa mzunguko huo.
Alisema kupitia utaratibu huo, timu nne za kutoka katika kila
kundi zilifanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho na kuingia nusu fainali
na hatimaye timu hizo ambazo zilicheza fainali hiyo.
Sambamba na hayo, Stendi FC waliibuka kidedea kwa kuzoa
kitita cha shilingi 150,000 kikombe na seti moja ya jezi, mshindi wa pili ni
Usalama FC ambao nao waliambulia shilingi 150,000 na seti moja ya jezi wakati
mshindi wa tatu Jeboyebo FC walinyakua shilingi 100,000 na mpira mmoja.
Timu nyingine ambazo zilishiriki katika ligi hiyo kuwa ni;
Tunduru star FC, Majengo FC, Liver Combain FC, Tiger FC, Joka FC, Mambo mazuri
FC, Veteran FC, Jobe FC na Red Scorpion FC na kwamba mgeni rasmi katika
mashindano hayo alikuwa ni Katibu tawala wa wilaya ya Tunduru, Ghaibu Lingo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Alli Mpenye alisema katika awamu ya kwanza zoezi
hilo lilihusishwa katika kata tano za Mgombasi ambapo watu waliojiandikisha
walikuwa 5,186, Namtumbo 9,041, Likuyu 4,952, Rwinga 7,586 na kata ya Luegu
watu waliojiandikisha walikuwa 4,064.
Mpenya alifafanua kuwa hivi sasa wanaendelea na kata
nyingine, na kwamba wamelazimika kufanya kwa wamu kutokana na ufinyu wa vifaa
ikiwemo mashine ya kuandikishia wapiga kura (BVR) ambapo baadhi yake
zilizoletwa na tume ya taifa ya uchaguzi ni mbovu na hushindwa kufanya kazi
ipasavyo na kulazimika kutumia mashine chache zilizopo ambazo hufanya kazi.
Alieleza kuwa baada ya kumaliza kazi hiyo ya uandikishaji
katika kata hizo, zoezi hilo litaendelea tena katika kata ambazo zipo pembezoni
mwa wilaya hiyo ambazo ni Ligera, Lusewa, Mgazini na kata ya Msisima.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, awali kazi hiyo ilianza kwa
kusuasua kwa kile alichoeleza kuwa mwitikio mdogo wa wananchi wenyewe na baada
ya kuwafikia taarifa za bkutosha katika maeneo yao ndipo walianza kujitokeza
kwa wingi.
Asasi za kiraia, wananchi na vyama vya siasa, Mpenye
amevipongeza kwa jitihada yao ya kupita kuhamasisha zoezi hilo ili watu
wakajiandikishe na ndio maana wengi wao hivi sasa katika vituo husika wilayani
humo, wanahamasa kubwa ya kutekeleza zoezi hilo ili utakapofika uchaguzi mkuu
ujao waweze kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayemataka awaongoze, kwa
nafasi ya Rais, Mbunge na Diwani.
No comments:
Post a Comment