Na Kassian Nyandindi,
Nyasa.
MSHAURI na Mwakilishi wa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Kari
Leppanen amefanya ziara ya siku mbili Mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.
Mwakilishi wa Balozi wa Finland Tanzania, Kari Leppanen. |
Akihojiwa juzi kwenye Hoteli ya kitalii ya Watawa wa Mtakatifu
Vincent iliyopo katika fukwe za Kilosa mjini Mbambabay wilayani humo, alisema kuwa
ameshangazwa na vivutio vya utalii ambavyo ni vya kipekee na adimu havipatikani
sehemu nyingine yoyote Duniani vilivyopo katika ziwa hilo.
Balozi huyo alisisitiza kuwa iwapo vivutio hivyo
vikiendelezwa vitafungua fursa kubwa ya uwekezaji na utalii kwa wananchi wa
eneo hilo na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Miongoni mwa vivutio vilivyopo katika ziwa Nyasa ni fukwe za
asili, visiwa ambazo samaki wa mapambo aina zaidi ya 400 huzaliana kwa wingi, milima
ya Livingstone, mawe ya ajabu kama vile jiwe la Pomonda na vivutio vingine vya
Ikolojia na Utamaduni.
No comments:
Post a Comment