WATAALAMU wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku
ya Jumapili walifanikiwa kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka kwa
miaka mingi na lilikuwa limeunganishwa wakati wa Vita kuu ya pili ya dunia.
Bomu hilo ambalo ni la tani 1.4 kutoka Uingereza
liligunduliwa katika eneo la ujenzi siku ya Jumatano.
Habari hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000
ambao walikuwa wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu
hilo kuteguliwa.
Hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu
kutokea kwa Vita hivyo nchini Ujerumani na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya
maafisa wa serikali.
Maeneo ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa
Westend pamoja na hospitali kadhaa, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika
Benki kuu ya Ujerumani.
Inaaminika kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa
vita kuu ya pili ya dunia ambayo hayakulipuliwa ambayo yametapakaa kote
Ujerumani.
No comments:
Post a Comment