Kenya. CHAMA cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali tukio
la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu
Lissu.
Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua wanasheria
wote wa Kenya.
“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye
gari lake mjini Dodoma, kwa kweli imetushtua sana na inahuzunisha,” amesema
katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
“Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa
wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla. Tunasikitika kwa uvunjifu wa
sheria uliofanyika,’’ amesema.
Amesema kuwa Lissu anafahamika kwa kutetea haki za binadamu,
hivyo wanasheria wote wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake na
Mungu atamsaidia atarudi katika hali yake ya kawaida.
Mwananchi:
No comments:
Post a Comment