Dar es Salaam.
MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea yupo
mikononi mwa polisi akisubiri mchakato wa kusafirishwa kupelekwa mjini Dodoma
kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Saed Kubenea. |
Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumanne, Kubenea
amesema yupo katika kituo cha polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni na
akisubiri utaratibu wa safari ya kwenda Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kama Spika
wa Bunge Job Ndugai alivyoagiza.
Kubenea amesema awali kabla ya kushikiliwa alikwenda
kujisalimisha polisi katika kituo hicho kisha aliambatana na askari hadi Katika
Hospitali ya Aga Khan ambako alitakiwa kwenda kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha
MRI.
“Baada ya kipimo kukamilika daktari alishauriwa nipumzike,
lakini askari wakaamuru niondoke na kurudi Oysterbay. Hapa ninapozungumza na
wewe nipo kituo nikisubiri kusafirishwa kwenda Dodoma,”amesema Kubenea na
kuongeza kuwa;
“Hata hivyo, daktari ameshauri nisisafiri kwa njia ya
barabara kutokana na matatizo ya mgogo niliyokuwa nayo hivyo nasubiri utaratibu
hapa,” amesema mbunge huyo.
Akizungumzia kushirikiliwa kwa Kubenea, Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo lilikuwa na
hati ya kukamatwa kupelekwa Dodoma kwa mbunge huyo ndiyo maana yupo mikononi
mwao.
“Atapelekwa lini, atatoka saa ngapi au atasafirishwa kwa njia
gani hilo mimi sijui ila atapelekwa Dodoma chini ulinzi wa polisi. Ukishakuwa
na hati ya kukamatwa lazima utakaa mahabusu tu,”amesema Kamanda Mambosasa.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema;“Kwanza sijui kama yupo
polisi ndiyo kwanza nakisikia kwako,” alieleza.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika kujua
kama wajumbe wajumbe kamati yake, bado wapo Dodoma baada ya kikao cha Bunge
kuhairishwa wiki iliyopita alijibu;
“Shughuli za kamati yangu hazifanyika katika magazeti, sisi
tunafanya kimyakimya kisha tunamkabidhi Spika wa Bunge,” alijibu Mkuchika kisha
kukata simu.
Source: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment