Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
SERIKALI wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma imesema kwamba,
wanakubaliana na utendaji kazi wa Kituo cha msaada wa Kisheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kilichopo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, kufuatia Wasaidizi
wake wa kisheria (Paralegals) kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa misingi na
taratibu husika zilizowekwa.
Hayo yalisemwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Mhandisi Gilbert Simya
alipokuwa akizungumza Ofisini kwake na wageni kutoka Ubalozi wa Sweden na
Norway Tanzania ambao ndiyo Wafadhili wanaoendesha na kufanikisha shughuli za
msaada wa kisheria katika Kituo cha sheria na haki za binadamu wilayani hapa.
Leo Septemba 20 mwaka huu Wafadhili waliotembelea kwa Katibu
tawala huyo ni Anette Widholme Bolme, Alexandra Hallqvist na Ludviq Bontell ambao
ni Meneja wa miradi Ubalozi wa ufalme Sweden na Victor Mlunde wa kutoka Ubalozi wa ufalme wa Norway.
“Kwa niaba ya serikali Mbinga binafsi nakubaliana na utendaji kazi
mzuri wa hawa wenzetu Paralegals, kwa sababu asilimia kubwa ya watu wetu wa
Mbinga hawajui masuala ya kisheria na namna ya kupata haki zao za msingi”,
alisema Simya.
Kwa upande wake Anette Widholme Bolme akihoji kwa niaba ya
wenzake alipotaka ufafanuzi juu ya namna Wasaidizi hao wa kisheria
wanavyoshirikiana na vyombo vya serikali wilayani humo, Katibu tawala huyo
alifafanua kuwa wamekuwa wakiishirikisha serikali ipasavyo hususan katika hata
mafunzo mbalimbali yanayotolewa pale wanapokuwa wakielimisha wananchi au jamii
katika eneo fulani.
Vilevile alipotaka kujua juu ya masuala gani ambayo
yameshamiri wilayani Mbinga na kuwa kikwazo katika kuleta migogoro katika
jamii, Simiya alisema kuwa kwa wilaya hiyo kumekuwa hasa na matatizo katika
masuala ya ardhi, familia (watoto), ndoa na makosa ya jinai ambayo wananchi muda mwingi
wanahitaji msaada wa karibu wa kisheria.
Kadhalika wageni hao walipozungumza na Afisa maendeleo ya
jamii wa wilaya hiyo, Paschal Ndunguru aliwaeleza kuwa watu wengi hivi sasa
wamekuwa wakikimbilia kwa Wasaidizi wa kisheria kituo cha Mbinga, kwa sababu ya
kupata huduma nzuri na kuona wanafanikiwa katika masuala yao.
“Hawa Wasaidizi wa kisheria wananchi hapa kwetu wamekuwa
wakiwakubali kwa utendaji wao mzuri wa kazi jinsi wanavyosaidia wanambinga
wenzao”, alisema Ndunguru.
Alisema kuwa halmashauri ya wilaya inatambua kuwa tatizo
kubwa linalokabili mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni ukosefu wa fedha za
kuweza kuendeshea shughuli za kusaidia wananchi, ikiwemo kufikisha elimu husika
katika jamii kama vile masuala ya kupambana na maambukizi mapya ya ugonjwa wa
Ukimwi (HIV), jinsia na kuzuia tatizo la watoto wa shule za sekondari wasiweze
kupata ujauzito.
Ndunguru alisema katika kupunguza matatizo hayo halmashauri
imekuwa ikitenga fedha katika bajeti zake kila mwaka na pale inapofanikiwa fedha
kidogo hupita kwa wananchi kuelimisha jamii namna ya kuweza kudhibiti hali hiyo.
(Family care)
Pamoja na mambo mengine, kwa upande wao wageni hao kwa nyakati tofauti waliahidi kuendelea kushirikiana na Wasaidizi wa kisheria wa wilaya ya Mbinga, ili kuweza kutatua migogoro mbalimbali ambayo inaendelea kuitesa jamii hasa kwa wale watu wanaoishi vijijini.
Pamoja na mambo mengine, kwa upande wao wageni hao kwa nyakati tofauti waliahidi kuendelea kushirikiana na Wasaidizi wa kisheria wa wilaya ya Mbinga, ili kuweza kutatua migogoro mbalimbali ambayo inaendelea kuitesa jamii hasa kwa wale watu wanaoishi vijijini.
No comments:
Post a Comment