Zitto Kabwe. |
Na Mwandishi wetu,
MBUNGE wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa
watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha
moto ulioteketeza nyumba yake.
Nyumba hiyo iliteketea jana Jumamosi alasiri na hakuna
madhara kwa binadamu yaliyotokea isipokuwa mali zote zilizokuwamo ndani
zimeteketea.
“Tumepata ajali kidogo, nyumba yangu ninayoishi katika eneo
la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii.
Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia”, aliandika Zitto katika ukurasa
wake wa Facebook.
Alisema analishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji, majirani
zake na wananchi wenzake kwa ushirikiano walioutoa ili kuzima moto huo.
“Kwa sasa Jeshi la Polisi wanafanyia kazi kujua chanzo cha
ajali hiyo.
Alisema kuwa anaomba wananchi wawe watulivu wakati Polisi
wanaendelea na uchunguzi husika.
Nyumba hiyo aliyoijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya
kwanza iko kiwanja kimoja na nyumba yake ya sasa.
Msaidizi wa Mbunge huyo, Nyembo Mustafa alisema Zitto hakuwa
anaishi kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyingine kubwa kwenye kiwanja
hicho.
No comments:
Post a Comment